Chifu wa Wayao atamba CCM itashinda Tunduru

Na Richard Mwaikenda, Tunduru.
CHIFU wa Kabila la Wayao, wilayani Tunduru, Sultani Kalolo ametamba kuwa atausambaratisha upinzani na kuhakikisha wagombea wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) watashinda kwa kura nyingi.
Chifu Kalolo, alitoa kauli hiyo katika  mkutano wa kampeni uliohutubiwa na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Ridhiwani Kikwete katika makazi ya chifu huyo eneo la Jakika,Jimbo la Tunduru Kaskazini.

"Kwanza nina uhakika katika Kata yangu ya Matemanga, CCM inachukua kura zote, pia nitahakikisha wagombea wote wa CCM wanashinda, kwani kila mtu anajua jinsi Serikali ya Awamu ya Nne ilvyotufanyia katika eneo letu, atakaye pinga atakuwa ni mwendawazimu na asiye na shukrani, pia atakuwa ana roho kama hiyo,"alisema Chifu Kalolo huku akishangiliwa na wanakijiji.

Alisema ili kudhihirisha hilo, tayari ameshaanza kampeni, kwani juzi alipokwenda Tunduru mjini, alipiga domo kidogo na watu waliokuwa wamepandisha bendera za Chama cha Wananchi (CUF),na punde baada ya kwenda na kurudi kutoka msikitini kuswali, alikuta tayari bendera sita zimeshashushwa.na kwamba anaamini akienda tena awmu ya pili zote zitaondolewa.

Pia Chifu, alitumia fursa hiyo kumtaka Mtoto wake, Omari Kalolo ambaye alichuana vikali katika kura za maoni za kuwania ubunge Jimbo la Tunduru Kaskazini, avunje makundi na kumuunga mkono mgombea aliyeshinda, Injinia Ramo Makani.

Baada ya kusema hivyo, Omar Kalolo na Injinia Makani walipita mbele  ya Chifu, wananchi pamoja na Ridhiwani na kuanza kukumbatiana kwa furaha na wote kuahidi kuwa tofauti zao zimekwisha na kuanza safari ya kusaka kura kwa pamoja.

Awali Chifu Kalolo, alimtambulisha Ridhiwani kwa wanakijiji na kusifia kuwa ujio wa Ridhiwani ni faraja na heshima kubwa kwao na kwamba wanatambua kuwa kwa kitendo hicho ni sawa kuhesabu kuwa Rais mwenyewe Jakaya Kikwete yupo pale.

Akihutubia katika mkutano huo, Ridhiwani ambaye yupo katika ziara ya kampeni ya kuweka mikakati ya ushindi wa kishindo kwa CCM, alisema kuwa wameamua kwenda kwa Chifu Kalolo, kutokanana chifu huyo ambaye ni mwanachama hai wa CCM, kuwa na umuhimu katika Jamii na kwamba waeona atawasaidia katika kinyang'anyiro hicho.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA