RIDHIWANI KUJENGA UPYA SHULE ALIYOSOMA NACHINGWEA

Ridhiwani kujenga upya shule aliyosoma
Na Richard Mwaikenda, Nachingwea,
MJUMBE wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa,Ridhiwani Kikwete,ametembelea Shule ya Msingi ya Matangini, Mjini Nachingwea, aliyosoma darasa la kwanza mwaka 1987 na kuahidi kujenga upya vyumba vya madarasa shuleni hapo.

Ridhiwani ambaye yuko katika ziara ya mikoa ya Kanda ya Kusini kufanya kampeni za kuweka mikakati ya kuipatia ushindi CCM katika Uchaguzi Mkuu, alitoa ahadi hiyo kwa walimu baada ya kuahirisha kwa  muda ziara hiyo na kuamua kutembelea shule hiyo na kusikitishwa na hali mbaya ya majengo ya vyumba vya madarasa na upungufu mkubwa wa madawati.
"Hali niliyoiona inasikitisha sana, baadhi ya vyumba vya madarasa tutavunja na kujenga upya na kazi hii itatekelezwa kabla ya mwisho wa mwaka huu. Nimeahidi lazima nifanye," alisema Ridhiwani huku akipigiwa makofi na walimu aliowakuta kwenye chumba cha walimu.
"
"Nataka nifanye kitu kikubwa hasa kwa heshima ya wazazi wangu.pia nitatoa vifaa vya michezo na madawati ili watoto washiriki kwenye michezo mbalimbali na kusomea kwenye mazingira mazuri tofauti na ilivyo sasa,"alisema Ridhiwani.
Akizungumza na walimu shuleni hapo, Ridhiwani alisema kuwa msomi hawezi kujiita kuwa ana digrii bila kukumbuka alikoanzia kusoma, na kwamba yeye asingeweza kujua kusoma bila shule ya Matangini.Alisoma hapo wakati babake, Rais Jakaya Kikwete akiwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Nachingwea 1986/1988.
 
Akitoa shukrani, Mkuu wa shule hiyo,Renard Mnungu, alisema kuwa yeye na walimu wenzie  wamefarijika sana na kwamba jambo hilo ni faraja kubwa kwa walimu na linawatia moyo wanafunzi.
Alisema kuwa hivi sasa majengo ya shule hiyo kwa asilimia kubwa yamechakaa, tofauti na walipokuwa wakisoma akina Ridhiwani,kwani licha ya uchakavu huo pia kuna upungufu wa madawati na vifaa vya miceozo.
Kabla ya kuondoka Ridhiwani, alipiga picha za kumbukumbu na walimu pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo. Pia alitumia fursa hiyo kwenda nyumbani kwa Mwalimu aliyemfundisha darasa la kwanza kumsalimia, lakini bahati mbaya alimkuta akiwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi.Alifika na kumjulia hali mwalimu huyo aitwaye Sophia Makong'o.
mwisho

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.