SAKENI KURA HADI VICHCOCHCORONI

Na Richard Mwaikenda, Newala

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, ambaye pia ni mgombea ubunge Jimbo la Newala, Kapteni msitaafu George Mkuchika, ametoa mwito kwa vijana wa chama hicho kutobweteka  katika kipindi hiki cha kampeni za Uchaguzi Mkuu, kwa  kubaki kusema kwa maneno kuwa watapata ushindi, bali wanatakiwa kwenda kwenye vijiwe,vijiji,kata kueleza utekelezaji wa ilani ya chama ili kukomba kura nyingi zitakazofanikisha ushindi wa kishindo.

Mkuchika alitoa mwito huo, alipopewa wasaa wa kujinadi katika mkutano wa ndani wa vijana wa chama hicho, uliohutuiwa na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa Chama hicho,UVCCM Taifa, Ridhiwani Kikwete, mjini Newala,akiwa kwenye mwendelezo wa ziara ya kampeni ya kuweka mikakati ya ushindi wa CCM.

"Ukitaka kutathmini uimara wa Taifa lolote Duniani, ni kuangalia msimamo wa vijana, na nguvu ya chama chetu inawategemea nyie vijana, hivyo mnatakiwa mtumie uwezo wenu kwenda walipo watu, yaani vijiweni, vijijini na kwenye  Kata kueleza sera nzuri za chama pamoja na utekelezaji wa ialani ya chama katika miradi mbailimbali inayogusa maisha ya kila ya jamii,"alisema Mkuchika huku akishangiliwa.

Aliema kuwa moja ya makosa wanayofanya wana CCM, ni kutokwenda kwa wananchi kuwaeleza ukweli kuhusu mafanikio ya Serikali ya Awamu Nne hasa kwa miradi iliyotekelezwa katika maeneo yao, kwamba Serikali imefanikisha ujenzi wa shule za sekondari, Zahanati, ujenzi wa visima vya maji na uboreshaji wa miundombinu zikiwemo barabara.

"Wananchi wa Newala hawawezi kukuelewa endapo, utawambia kuwa moja ya mafanikio ya ni ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe Mbeya, wao kwa asilimia kubwa hauwahusu, bali unatakiwa kuwaeleza ni miradi gani ya maendeleo imetekelezwa ndani ya maeneo yao,"alisema Mkuchika.

Pia kauli hiyo, imekuwa ikielezwa mara kwa mara na kiongozi vijana Taifa,Ridhiwani anapohutubia katika mikutano mbalimbali ya kampeni anayoifanya katika ziara yake, ambapo anawahimiza wana CCM na hasa vijana kwenda kuzisaka kura kwa mtindo wa nyumba kwa nyumba,kitanda kwa kitanda na shuka kwa shuka.

"Jamani nendeni kuzisaka kura vichochoroni, vijiweni, kwenye daladala, mashambani na popote panapowekana kuwaeleza ukweli juu ya mafanikio mbalimbali ya Serikali ya CCM, watu mtakaowakuta huko watawaelewa'na  hivyo CCM kujikusanyia kura nyIngi kwa wagombea wetu na hatimaye safari hii kupata ushindi wa kishindo,"alisema Ridhiwani alipokuwa katika ziara wilayani Ruangwa, Lindi.

Pia, Ridhiwani amekuwa akiwahimiza wana CCM na wananchi wenye mapenzi na CCM,kuhakikisha siku ya kupiga kura wanahamasishana kwenda kupiga kura kwa kila mmoja kumkumbusha mwenzie ikiwemo kuwasaidia wazee, wajawazito, walemavu na wagonjwa ili wafike kwa wingi kupiga kura zitakazoipatia CCM ushindi mnono wanaouita wa manyoya.
mwisho

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.