4x4

RIDHIWANI AKIHUTUBIA MKUTANO ULIODAIWA HAUKUFANYIKA IPOGOLO, IRINGA

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji la Baraza 

Kuu la UVCCM Taifa, Ridhiwani Kikwete akihutubia katika mkutano wa ndani wa kampeni za kuweka mikakati ya ushindi wa kishindo kwa CCM, Ipogolo, Iringa jana.

RIDHIWANI AHUTUBIA VIJANA IPOGOLO,IRINGA

Ridhiwani akuhutubia katika mkutano wa ndani wa kampeni ya kuweka mikakati ya ushindi wa kishindo katika ofisi ya CCM Kata  Ruaha, eneo la , Ipogolo, Iringa jana.

JESCA ASISITIZA AMEVUNJA MAKUNDI

Aliyekuwa miongoni mwa wagombea ubunge 12 Jimbo la Iringa

mjini, Jesca Msambatavangu akisisitiza katika mkutano huo

kuwa amevunja makundi na kuungana kuipigania CCM ili ishinde

kwa kishindo.Kutoka kushoto ni Ridhiwani Kikwete, Fadhil Ngajilo na Frederick Mwakalebela.

KIJANA AKICHANGIA MADA

Mmoja wa vijana walihudhuria mkutano wa ndani wa kampeni za

kuweka mikakati ya ushindi kwa CCM, akichangia mada katika

mkutano huo uliohutubiwa na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji

la Baraza  Kuu la UVCCM Taifa, Ridhiwani Kikwete jana katika

 ofisi za CCM Kata ya Ipogolo,Iringa.

MKUATANO ULIODAIWA KUTOFANYIKA IPIGOLO,IRINGA HUU HAPA

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Iringa,ambaye pia alikuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Iringa mjini katika kura za maoni, Fadhil Ngajilo akiwahutubia vijana wa Ipogolo, Iringa jana. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji la Baraza  Kuu la UVCCM Taifa, Ridhiwani Kikwete na Frederick Mwakalebela ambaye pia alikuwa miongoni mwa wagombea 12 wa katika kura za maoni.

RIDHIWANI AKILISHWA KEKI NA DAUD MSUNGU

RIDHIWANI AKIMLISHA KEKI KAMANDA MWAIKENDA

Ridhiwani akimlisha keki Daud Msungu

MWAKALEBELA AKILISHWA KEKI

RIDHIWANI AWAPATANISHA MBEGA NA MWAKALEBELA

Na Richard Mwaikenda, Iringa.

MJUMBE wa Kamati ya utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ridhiwani Kikwete, amewapatanisha Mgombea ubunge wa Jimbo la Iringa mjini, kupitia Chama hicho, Monica Mbega na David Mwakalebela aliyeenguliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, baada ya kuongoza katika kura za maoni.

Makada hao ambao makundi yao yamegawawinyiko, waliamua kuyavunja mbele ya Ridhiwani, uongozi wa CCM Iringa na wajumbe wa baraza hilo lililohudhuriwa na vijana wa makundi ya wagombea wote miongoni mwao wakiwmo wa wagombea wengine 10 walioshindwa.Jumla ya wanachama 12 waliwania nafasi hiyo, ambapo Mwakalebela aliongoza.

Ili kudhihirisha kwamba wamepatana, walikubali kupiga picha huku wakiwa wameshikwa mikono na Ridhiwani, kitendo ambacho kiliibua chereko chereko na shangwe katika kikao hicho kilichowashirikisha pia baadhi ya wazee makada wa chama hicho.

Baada ya kupewa fursa ya kuwasalimia wajumbe wa baraza hilo, Mwakalebela, alielezea kuwa baada ya kuenguliwa na NEC, alifuatwa na viongozi wa upinzania wakita ajiunge na vyama vyao, lakini alikataa kwani hakutaka kukigeuka chama chake.

"Nilifuatwa na viongozi wa Vyama vya upinzani kutaka niihame CCM na kujiunga na vyama vyao, lakini nilikataa kukigeuka chama changu, kwani nimekulia ndani ya chama hicho. Nilikuwepo CCM, nipo CCM na nitaendelea kuwa CCM," aliapa Mwakalebela huku akishangiliwa.

Mwakalebela, aliwaomba wote waliokuwa wanamuunga mkono wakati wa mchakato wa kura za maoni,kurudisha nyoyo zao na kuungana kumpigania kwa hali na mali mgombea wao Mbega ili ashinde kwa kura nyingi.

"Vijana ndiyo nguvu kazi, tuko vitani,naomba tuondoe tofauti zetu, tuungane pamoja na kuhakikisha mgombea wetu Mbega, Rais Kikwete na madiwani wanashinda kwa kura nyingi ili CCM ishike tena madaraka ya nchi,"alisema Mwakalebela.

Aliwaasa wanaCCM kutothubutu kuihama CCM, akidai kuwa ina sera nzuri yenye mafanikio kwa jamii, na kwamba wasijaribu kwenda kwenye chama ambacho sera na ilani zake hazifahamiki.

Awali, akihutubia katika baraza hilo, Ridhiwani, aliwataka wanaCCM, kabla ya kuamua kuwania uongozi ndani ya chama hicho, kujua kanuni na taratibu za uchaguzi ili kuepusha migogoro inayojitokeza baada ya matokeo.

"Kabla ya kuanza kugombea lazima uelewe taratibu za uchaguzi ndani ya chama, na kama hujui basi hupaswi kugombea.Kila mwanachama ana haki ya kugombea lakini tuwe na subira ya mapendekezo kutoka ngazi ya juu,"alisema Ridhiwani.

Ridhiwani, alipongeza kitendo cha Mwakalebela, kukubali matokeo na kuamua kuvunja makundi na kuungana na mgombea Mbega katika kampeni ambapo aliwataka wale wote waliokuwa wakimwamini na kumuunga mkono warudishe nyoyo zao wajenge umoja kwa kushiriki pamoja kwenye kampeni.

"Wana Iringa, kipindi hiki si cha kugawanyika, kwani tunataka tupate ushindi wa kishindo ili tuunde dola tutekeleze ilani yetu kwa maendeleo ya wananchi.Tusahau yaliyopita, tugange yaliyopo na yajayo, lazima tukipiganie chama chetu,"alisema Ridhiwani.

Naye, Mgombea ubunge Jimbo la Iringa mjini, Mbega, alikipongeza kitendo cha Mwakalebela cha kukubali kuvunja makundi na kuungana na yeye kwenye kampeni za kuhakikisha chama kinapata ushindi wa kishindo.
mwisho

RIDHIWANI AWAPATANISHA MBEGA NA MWAKALEBELA


Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza la Umoja wa Viajana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ridhiwani Kikwete (katikati), akiwatambulisha Monica Mbega (kulia) na Davidi Mwakalebela baada ya kuwapatanisha na kuvunja makundi katika kikao cha Baraza la Vijana mjini Iringa jana.Monica ni mgombea ubunge Jimbo la Iringa mjini na Mwakalebela alienguliwa kuwania nafasi hiyo.

5774
Wajumbe wa Baraza la Vijana wa CCM, Iringa mjini, wakishangilia baada ya Mgombea ubunge Jimbo la Iringa mjini, Monica Mbega na David Mwakalebela aliyeenguliwa kuwania nafasi hiyo, kupatanishwa na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ridhiwani Kikwete mjini Iringa jana.

Mgombea ubunge Jmbo la Iringa mjini, Monica Mbega (kulia), akikumbatiana kwa furaha na David Mwakalebela baada ya kuahidi kuvunja makundi mbele ya Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza la Umoja wa Viajana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ridhiwani Kikwete katika kikao cha Baraza la UVCCM, Iringa mjini jana. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)

Mgombea ubunge Jmbo la Iringa mjini, Monica Mbega (kulia), akikumbatiana kwa furaha na David Mwakalebela baada ya kuahidi kuvunja makundi mbele ya Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza la Umoja wa Viajana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ridhiwani Kikwete (kushoto) katika kikao cha Baraza la UVCCM, Iringa mjini jana. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)

JK NDANI YA MASWA SHINYANGA


  
Maswa mjini 1.  Mamia ya wananchi wa mji wa Maswa, mkoani Shinyanga wakisikiliza kwa makini hotuba ya kampeni iliyokuwa inatolewa na Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Kikwete tarehe 27.9.2010.
 


Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Kikwete akinadi sera zake kwa wananchi wa mji wa Maswa katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini humo tarehe 27.9.2010.
Add caption

PINDA AUNGURUMA UN

Mkuu, Mizengo Pinda akilihutubia Baraza  Kuu la Umoja wa Mataifa Mjini New York  alikomwakilisha Rais Jakaya Kikwete Septemba 27, 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  

     2718  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Wanachuo wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Aiowa nchini Marekani wakti alipotembelea Chuo hicho Septemba 25, 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

DK. BILAL ATINGA MBEYA


03:- dK. Bilal, akiwahutubia wananchi wa Wilaya ya Mbeya mjini leo katika eneo la Kibondenyasi.
Wananchi wa Kata ya Nsalaga Kibondenyasi, wakiwa na mabango yenye ujumbe wa kukinadi chama cha Mapionduzi, wakati wakimsikiliza Mgombea Mwenza wa urais  wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akifanya mkutano wa kampeni eneo hilo Mkoani Mbeya leo Sept 28

RIDHIWANI AKARIBISHWA KIAINA ILEJE

ILEJE INAVYOONEKANA KUTOKA KWENYE VILIMA

RIDHIWANI AZAWADIWA KUKU MWENYE UWEZO WA KUTAGA MAYAI 800


Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Ileje, Hebroni Kibona,akimkabidhi zawadi ya kuku,Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)Taifa,Ridhiwani Kikwete baada ya kufanya mkutano wa kufanikisha ushindi wa kishindo wa chama hicho, juzi katika Kata ya Kinyala, Rungwe.

Wanachama wa Shirikisho la walimu, wanachama wa CCM, wakiwa katika mapokezi ya msafara wa Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)Taifa, Ridhiwani Kikwete, ulipowasili Ileje, Mbeya juzi.

Wanachama wa Shirikisho la walimu, wanachama wa CCM, wakiwa katika mapokezi ya msafara wa Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)Taifa, Ridhiwani Kikwete, ulipowasili Ileje, Mbeya juzi.
Ridhiwani akiwa na kikosi kazi wakivinjari matukio mbalimbali ya ziara yao kwenye Blogu ya Kamanda wa Matukio, juzi mjini Mbalizi wakitokea Chunya.

RIDHIWANI AMKABIDHI FULANA SHEIKH MKUU MBEYA


Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)Taifa,Ridhiwani Kikwete,akimkabidhi Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Mohammed Mwansasu zawadi ya fulana yenye ujumbe wa kumkampenia Rais Jakaya Kikwete, juzi mjini Mbalizi,Mbeya. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
5326

Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)Taifa,Ridhiwani Kikwete, akimkabIdhi Katibu wa UVCCM Kata ya Mkwajuni, Charles Mwaniwe moja kati ya baiskeli 180 zilizotolewa na UVCCM Taifa kwa Kata 180 mkoani Mbeya.Ridhiwani alikuwa Wilayani Chunya kwa ziara ya kampeni ya kuweka mikakati ya ushindi kwa CCM, juzi.

Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)Taifa,Ridhiwani Kikwete, akihutubia katika mkutano wa kampeni za kuweka mikakati ya ushindi wa kishindo wa CCM, juzi katika Mji wa Mkwajuni, Jimbo la Songwe, Chunya, Mbeya.

DK SIAME ASHINIKIZWA KUVUNJA MAKUNDI MBOZI

Na Richard Mwaikenda, Mbozi.

MGOMBEA ubunge Jimbo la Mbozi Magharibi, Dk. Lukas Siame,ametakiwa kuvunja makambi  na kuwaomba radhi wananchi aliowakosea wakati wa mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ili kujenga umoja na mshikamano utakaokifanya chama kishinde kwa kishindo katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 31,mwaka huu.

Alishinikizwa kufanya hivyo na uongozi wa CCM Wilaya ya Mbozi na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Ridhiwani Kikwete wakati wa mkutano wa ndani wa kuweka mikakati ya kukipatia chama hicho ushindi wa kishindo uliofanyika juzi mjini hapa.

Ililazimika kumwambia hivyo, baada ya kubaini  kuendelea kuwepo  kwa makundi katika baadhi ya Tarafa  jimboni humo,hali ambayo inaweza kuhatarisha chama hicho kukosa  baadhi kura muhimu zinazohitajika kukipatia chama hicho ushindi wa kimbunga.

Jambo linginne lilowashitua ni kitendo cha mgombea huyo, kutamka wazi katika mkutano huo, kuwa yupo tayari kukosa kura za watu wasiokubali kuvunja makundi na kuungana naye katika kampeni na kwamba ana uhakikia kupata kura kwa watu wengine wanaomkubali.

"Naamini makundi yaliyojitokeza wakati wa kura za maoni tulizimaliza, na endapo kama kuna kundi halikubali kuvunja makundi , basi mimi niko tayari kuzikosa kura zao,lakini tutazipata kwa wengine wanaoniunga mkono,"alisema Dk. Siame..

Akihutubia katika mkutano huo, uliohudhuriwa pia na Mgombea ubunge jimbo la Mbozi Mashariki kupitia chama hicho, Godfrey Zambi, Mgeni rasmi, Ridhiwani alielezea kuwa si dhambi wakati wa kipindi cha mchakato wa uchaguzi wa kura za maoni kuibuka makundi, na kudai kwamba  hiyo ni demokrasia ndani ya CCM, lakini makundi hayo yanatakiwa kuvunjwa mara moja anapotangazwa mshindi.

"Si dhambi wakati wa kipindi cha uchaguzi, kuwepo mgawanyiko maana hiyo ndio demokrasia ndani ya CCM,kwani si lazima unayempenda wewe basi kila mtu ampende,lakini utake usitake mwana CCM atakayeshinda katika mchakato huo na ambaye uongozi wa juu utamjadili na  kurudisha jina lake,basi huyo ni wetu wote inatakiwa tumpiganie ashinde," alisema Ridhiwani.

"Kipindi cha kura ya maoni kilishapita, kinachotakiwa sasa ni wanaCCM kuwa na umoja pamoja na mshikamano utakaotuwezesha kukipatia chama chetu ushindi wa kishindo usioelezeka,"alisema Ridhiwani huku akishangiliwa. .

Ridhiwani, alikemea kitendo cha wapambe kuendelea kuwadhihaki wenzao waliokuwa kwenye kambi iliyoshindwa, na kuwataka waache mara moja tabia hiyo kwani haimsaidii mgombea,mwananchi na hata chama chenyewe.

"Wagombea na wapambe acheni kuwadhihaki na kuwakejeli wenzenu walioshindwa, tabia hiyo siyo nzuri, inawafanya wakichukie chama, tusahau yaliyotokea, tujirekebishe tulipokosea, tujenge umoja kwani kidole kimoja hakivunji chawa,"aliwaasa Ridhiwani.

Naye Mgombea ubunge Jimbo la Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi, alitamba kuwa kwa jinsi anavyoendesha kampeni zake ni dhahiri CCM jimboni humo itapata ushindi si chini ya asilimia 90,kwa vile katika kampeni amewashirikisha watu bila kujali anatoka kundi gani na kwamba hana kundi bali alilobakia nalo ni kundi moja tu la CCM.

Pia, Mwenyekiti wa UVCCM, Wilaya ya Mbozi,Jobu Kabinja, alisisitiza kauli zilizotolewa na baadhi ya viongozi kwa kumtaka Dk. Siame asiendelee na tabia ya kuzikataa kura za watu wasiotaka kuvunja makundi, kwa vile kura hizo wanazihitaji.

Naye Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo,Aloyce Mdaravuma, aliungana na viongozi wenzie, kwa kusema kuwa, wataungana na Dk. Siame kwenye kampeni kwa kuziomba kura kwa unyenyekevu hata kwa kulala chini mpaka kieleweke.

"Tutaingia kiume kwenye kampeni kwa kuzisaka kura katika Kata,vitongoji na nyumba kwa nyumba, hatutaki hata kura moja ipotee, kwani kura siyo zako ni za CCM,"alimazia kusema Mdaravuma.
mwisho

RIDHIWANI ATAWAZWA KUWA CHIFU WA WANYAKYUSA


Machifu wa kinyakyusa Ernest Mwailemale (kushoto) na
Glasswell Mwakalukwa wakimvisha golole,Mjumbe wa Kamati ya
utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM
(UVCCM)Taifa,Ridhiwani Kikwete, alipotawazwa kuwa chifu wa
kinyakyusa na kuitwa Chifu Mwailemale juzi katika mkutano wa
kampeni za ndani za kuweka mikakati ya kuipatia CCM ushindi
wa kishindo,juzi katika Kata ya Ipinda, Kyela. (PICHA NA
RICHARD MWAIKENDA)

Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa
Vijana wa CCM (UVCCM)Taifa,Ridhiwani Kikwete, akikabidhiwa
na Chifu Lufingo Mwakitalu mkuki ikiwa ni ishara ya ulinzi
imara, baada ya kutawazwa kuwa Chifu wa kinyakyusa juzi
katika mkutano wa kampeni za ndani za kuweka mikakati ya
kuipatia CCM ushindi wa kishindo,juzi katika Kata ya Ipinda,
Kyela.Amepewa jina la Chifu Mwailemale.Kulia ni Chifu
Glasswell Mwakalukwa. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
Chifu Mwailemale akishangiliwa alipokuwa akihutubia

Chifu Mwailemale.Ridhiwani Kikwete akiwa amekalia
kigoda baada ya kutawazwa

Chifu Mwailemale akihutubia baada ya kutawazwa.

Chifu Mwailemale akihutubia baada ya kutawazwa.

RIDHIWANI APEWA ZAWADI YA NDIZI,VIAZI NA KUU RUNGWE

Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa
Vijana wa CCM (UVCCM)Taifa,Ridhiwani Kikwete, akikabidhiwa
zawadi ya mkungu wa ndizi baada ya kuhutubia katika mkutano
wa ndani wa kupanga mikakati ya ushindi wa kishindo kwa CCM,
katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 31, mwaka huu, juzi katika Kata
ya Kinyala, Rungwe.Alikabidhiwa mikungu miwile, kuku na
gunia la viazi mviringo.(PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)

RIDHIWANI ATINGA CHUNYA


Ridhiwani akiwatambulisha kwa wananchi, mgombea ubunge jimbo la Lupa, Victor Mwambalaswa kulia na mgombea Udiwani Kata ya Mbegani,Bosco Mwanginde leo asubuhi katika jimbo la Lupa,Chunya.

Ridhiwani akihutubia baada ya kufungua tawi la wakereketwa wa CCM, katika Kata ya Mbugani,Chunya.

Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)Taifa,Ridhiwani Kikwete,akivishwa skafu alpowasili leo asubuhi katika Jimbo la Lupa, Chunya kuendeleza kampeni za ushindi wa kishindo kwa CCM.

Peter Haule wa Taasisi ya Vijana Zaidi, akishangaa milima ya Kawetele

Kikosi Kazi kinachoongozwa na Ridhiwani, kikipata changamoto ya usafiri kwa moja ya magari yalioyopo kwenye msafara kupata pancha, karibu na Kilele cha Mlima Kawetele leo asubuhi.
Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa
Vijana wa CCM (UVCCM)Taifa,Ridhiwani Kikwete, akiwa na
Kikosi Kazi cha kampeni ya kuhakikisha ushindi mkubwa kwa 
CCM, kilipofika katika ubao unaoonesha barabara pekee nchini
iliyopita katika kilele cha mlima Kawete, Mbeya. Kikosi
hicho kilikuwa kinaelekea Chunya. 
Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa
Vijana wa CCM (UVCCM)Taifa,Ridhiwani Kikwete, akiwa na
Kikosi Kazi cha kampeni ya kuhakikisha ushindi mkubwa kwa 
CCM, kilipofika katika ubao unaoonesha barabara pekee nchini
iliyopita katika kilele cha mlima Kawete, Mbeya. Kikosi
hicho kilikuwa kinaelekea Chunya. 

KIKOSI KAZI SAFARINI CHUNYA

Kamanda Mwaikenda,akiwa na vijana wa Taasisi ya Vijana Zaidi, Peter Haule na Omar Matulanga katika ubao unaoelezea barabara pekee nchini iliyopita katika kilele kirefu eneo la Mlima Kawetele mpakani mwa Wilaya ya Mbeya Vijijini na Chunya
Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)Taifa,Ridhiwani Kikwete (katikati), akiwa na kikosi kazi cha kampeni ya kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo, mjini Mbeya leo asubuhi kabla ya kutwanga kiguu na njia kuendelea na zaiara yao wilayani Chunya. baadhi yao ni vijana kutoka mkoani Mbeya . Aliyevaa jaketi la kazi ni Kamanda Richard Mwaikenda ambaye ni Mwandishi wa habari wa msafara huo.
Ridhiwani Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa Uomja wa Wajasiriamali na Wavuja Jasho mkoani Mbeya (UVIWAMBE), baada ya kufanya nao mkutano jana Uyole, Mbeya . Wanachama hao ambao ni wakereketwa wa chama cha mapinduzi wameahidi kukipigia chama hicho kura nyingi wakati wa uchaguzi mkuu.

WEB YA JK NA DK BILAL HII HAPA

                                                         Habari zenu Ndugu wapendwa,

Tunayofuraha kubwa kuwafahamisha ya kwamba tovuti maalumu na rasmi ya Mhe. Jakaya M. Kikwete na Dr. M. Gharib Bilal sasa inapatikana kwenye mitandao:

www.kikwete2010.co.tz

Tembelea tovuti hii maalumu ya Mgombea Uraisi na Mgombea Mwenza kwa tiketi ya CCM mwaka 2010 upate habari mbalimbali kama:

· Wasifu wa Wagombea – Mhe. Jakaya M. Kikwete na Dr. Mohammed Gharib Bilal.

· Mafanikio katika sekta mbalimbali.

· Sera na Malengo 2010 – 2015.

· Ratiba za kampeni.

· Hotuba maalumu.

· Matoleo ya Habari.

· Video na picha.

· Mitandao ya Facebook,Twitter na Youtube.

Kupitia tovuti hii na mitandao yake utaweza kupata taarifa mbalimbali na kutoa maoni yako.

“ PAMOJA TUZIDI KUSONGA MBELE”

RIDHIWANI ATUA MBEYA , CHIFU AMKABIDHI ZAWADI YA KUKU


Mwenyekiti wa Muungano wa Machifu Mbeya, Shayo Masoko (kulia) akimkabidhi Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ridhiwani Kikwete zawadi ya kuku wakati wa mkutano wa kampeni za ndani za chama hicho, Mbalizi, mkoani Mbeya juzi.(PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ridhiwani Kikwete akikumbatiana kwa furaha na Mgombea ubunge Jimbo la Mbeya mjini kupitia CCMM Benson Mpesya baada ya kunadi wakati wa mkutano wa kampeni za ndani za chama hicho, Mbalizi, mkoani Mbeya juzi.(PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)