ASKOFU;WASIOWAAMINIFU WAJIONDOE SERIKALINI

MWENYEKITI wa Baraza la Maskofu wa Kanisa la Mennonite Tanzania, Askofu Stephan Mang'ana amewataka viongozi wasio waadilifu kujiondoa ndani ya Serikali ambao siyo waadilifu kujiondoa katika nafasi zao za uongozi. Askofu Mang'ana yasema hayo jana jijini Mwanza alipokuwa akihubiria katika ibada ya kumsimika Askofu Mteule Albert Jella Randa, sherehe zilizohudhuriwa pia na Rais Jakaya Kikwete ambaye ni mara yake ya kwanza kufika mkoani Mwanza tangu alipochaguliwa kuliongoza taifa kwa awamu ya pili.
Kiongozi huyo wa kanisa alidai kuwa hakuna haja kwa kiongonzi kung'ang'ania madarakani wakati hana uwezo wa kuongoza huku akimtwisha Rais Kikwete mzigo wa malalamiko ya wananchi ambao sio wake. “Nawahesimuni sana viongozi wetu, lakini kwa hili mtanisamehe. Nawaombeni mtoke kwa sababbu mmeshindwa kuwatumikia wananchi waliowapatieni dhama ya kuwa viongozi na badala yake mnaonekana majimboni kwenu wakati wa kuenda kuomba kura”alisema Mangana.
Akizugumzia sifa za kiongozi askofu huyo alisema kuwa kiongozi anapaswa kufahamu matatizo wanayopata wananchi na kuwa mstari wa mbele kuyatafutia ufumbuzi. Alisema kuwa kiongozi anapaswa kuelewa alama za nyakati ili kuondoa matabaka katika jamii ambayo imekuwa ikihangaika bila ya kujua hatima ya maisha yao ikibakia na maswali yasiyo na majibu kutokana na ugumu wa maisha.
Askofu Mang'ana alisema kuwa ni muhimu kwa kiongozi kujitoa kafara kwa kundi la watu anaowaongoza huku akitoa mfano wa Mussa katika Biblia alipokuwa akiwaongoza wana wa Israel.
“Mabadiliko ya kijamii yatatokea endapo viongozi wetu wataacha ubinafsi na kuitumikia jamii yao ikiwa pamoja na kukabilina na changamoto katika sehemu anayoongaza,”alisema Mangana.
Alisema kuwa kama ilivyokuwa kwa Mussa aliyepiga magoti mbele ya Mungu wake na kumwambia kuwa hana sauti juu ya watu anaowaongoza kwa kuwa ana mdomo mzito, basi iwe hivyo kwa viongozi kurudi kwa Rais Kikwete aliyewateua na kumwambia majukumu aliyowapa hawayawezi.
Askofu huyo alionyesha kusikitishwa na jinsi rasilimali za nchi zinavyoteketea kutokana na usimamizi mbaya wa viongozi walio madarakani na migomo inayotokea kila mara.
“Tanzania haikupaswa kuwa na migomo, badala yake watu wanaweza kukaa mezani na kusuluhisha matatizo yao. Nasikitika kuona mtoto mdogo yupo katikakati ya maandamano na bango kubwa tunawafundisha nini watoto wetu?,”alihoji askofu huyo.
Alimwomba askofu mteule Randa kuwa mtumishi wa wananchi badala ya kuwa kiongozi wa wananchi na kuwa mstari wa mbele katika kuliongoza kanisa.
Kwa upande wake, Rais Kikwete alisema kuwa Serikali imetenga Sh70 bilioni kwa ajili ya ruzuku kwa hospitali za taasisi za kidini ili ziweze kutoa huduma nzuri kwa jamii na kudumisha uhusiano wao na serikali.
Alisema kuwa madhehebu ya dini yanatoa mchango mkubwa kwa jamii na taifa kwa kuchangia katika kutoa elimu na huduma za kiafya akisema kuwa yeye pamoja na viongozi wenzake wanaheshimu mchango wa taasisi hizo za kidini.
Akitoa taarifa kuhusu dawa za kulevya nchini, Rais Kikwete iliziomba taasisi za dini kuongeza juhudi katika kukemea tatizo hilo huku akibainisha kuwa mkoa wa Mwanza unaongoza kwa kuwa na watumiaji na wauzaji wa dawa hizo huku mkoa wa Mara ukiongoza kwa kulima bangi.
Alisema katika kipindi cha mwaka 2010, kilo 12,196 za dawa hizo zilikamatwa huku Mkoa wa Mwanza ukiongoza kwa kukamata kilo 268 na kuongeza kuwa wanaothirika ni vijana wenye umri wa miaka 15-30 ambao ni nguvu ya taifa.
Rais Kikwete aliwaasa Watanzania kuwa macho na watu wenye lengo la kuvuruga amani ya nchi kwa madai kuwa watu hao hawapo tayari kuona Tanzania ikiwa na amani wakati kwao kuna machafuko.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI