CCM YAKOMBA 172 WA CHADEMA SINGIDA

SIKU moja baada ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Nape Mnauye kuanika ufisadi wa Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wake Dk. Wilbroad Slaa, wanachama 172 wakiwemo Makatibu Kata wawili mkoani Singida wamekikimbia chama hicho na kujiunga na CCM.
Waliotangaza kukihama Chadema ni aliyekuwa Katibu katika kata ya Urugu, Leonard Peter alikimbia na wanachama 150 na Joseph Peter aliyekuwa wa Kata ya Kyengege ambaye ameondoka na wanachama 22.
Hatua ya viongozi na wanachama hao wa Chadema kukimbia chama hicho waliitangaza, juzi, kwenye mkutano wa kutambulisha Sekretarieti mpya ya CCM uliofanyika katika kijiji cha Makunda, Kyengege jimbo la Iramba Magharibi mkoani hapa na kukabidhi kadi zao na za wenzao 172 kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM, John Chiligati na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) CCM, Nape Nnauye.
Wanachama hao wa Chadema walichukua hatua hiyo juzi, ikiwa ni siku moja, baada ya wengine 150 na Mwenyekiti wao wa chama hicho kata ya Msisi, Athumani Rajabu, kutangaza kukimbia na kujiunga na CCM katika mkutano wa kutambulisha wajumbe wa Sekretarieti ya CCM uliofanyika Stendi ya zamani ya mabasi mjini Singida, Jumatano wiki hii.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Stendi Kuu ya mabasi mjini Singida, Nape aliwashushia tuhuma nzito za ufisadi Dk. Slaa na Mbowe kwamba wamekuwa wakitafuna mamilioni ya fedha ambazo wamekuwa wakishinikiza kulipwa na Chadema kwa njia mbalimbali.
Katika mkutano huo, Nape alisema kwamba Dk. Slaa ameshinikiza kulipwa mshahara wa sh. milioni 7 kwa mwezi ambazo ni kiasi kikubwa kuliko mshahara wa mbunge wa sh. milioni 6 ambao Dk. Slaa amekuwa akilalamika kuwa ni kiasi kikubwa.
Nape pia alisema Mbowe ameshinikiza na kufanikiwa kuiuzia Chadema malori matatu aina ya Fuso kwa zaidi ya Sh. milioni 480, huku malori hayo yakiwa yamekwishatumika kwa muda mrefu.
Akizungumza aliyekuwa katibu wa Urugu, alisema, amechukua uamuzi huo baada ya kustushwa na ufisadi wa viongozi wa Chadema ambao alidhani ni wasafi kiasi kwamba Chadema iliposhindwa kutoa fedha wakati wa uchaguzi mkuu alijitolea mali zake kusaidia chama hicho kishinde udiwani katika kata hiyo ambapo kilifanikiwa ikiwa ni kata pekee iliyochukuliwa na upinzani katika jimbo la Iramba Magharibi.
Kingu alisema kutokana na imani aliyonayo kwa Dk. Slaa na Mbowe aliuza ng'ombe wake 17 na kuutumia mtaji wa biashara zake wa sh. milioni 4, kusaidia Chadema kifanye vizuri, kiasi kwamba aliishiwa uwezo wa kifedha na sasa amefilisika.
Alisema, baada ya kuishiwa wakati kampeni zikiendelea alimuomba Dk. Slaa, Chadema impatie fedha kwa ajili ya kuendelea kusimamia uchaguzi huo, lakini akamwambia akope kwa wafanyabiashara wenzake na atarejeshewa baada ya uchaguzi, akakopa.
"Lakini cha kushangaza tangu uchaguzi umalizike licha ya Chadema kushinda udiwani katika kata yetu hadi leo Dk. Slaa hajaja kunipa fedha zangu walau zile nilizokopa au hata kutupongeza kuleta ushindi, badala yake anafanya maandamano kwenye miji mikubwa tu ambako anajua atapata fedha ", alisema Kingu.
Alisema, alichobaini katika Chadema hakuna siasa za kweli bali ni mradi wa baadhi ya viongozi hasa Slaa na Katibu Mkuu, Freman Mbowe, kusaka fedha ndiyo sababu wanapenda sana maandamano kwa kuwa kila wanapoyaandaa na kuyafanya kuna harambee za siri ambazo hufanyika kuwapa fedha.
Katika mkutano huo, CCM ilikabidhi kadi kwa wanachama 80 wapya wa ambapo Naibu Katibu Mkuu, Chiligati aliwakabidhi kadhi kadi wanachama kumi kwa niaba ya wenzao.
Akiwapokea, Chiligati aliwatakaa watu kuacha kubabaika na kujiunga na vyama vya upinzani kama Chadema kwa kudhani watapata manufaa wao binafsi au taifa, badala yake waendelee kuiamini CCM hasa wakati huu ambapo imejivua gamba.
Chiligati alisema baada ya kujivua gamba, CCM itahakikisha yale maudhi ya hapa na pale yaliyokuwa yakiwakera wananchi na hata wanachama kiasi cha kwenda kujitosa kwenye upinzani kusikokuwa na matumaini sasa basi.
Katika ziara hiyo, wajumbe wa Sekretarieti hiyo waliofuatana mbali ya Chiligati na Nape, ni Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba na Katibu wa NEC, Oganaizesheni Asha Juma Abdallah.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*