Fifa yawasimamisha Bin Hammam na Warner

Mohamed Bin Hammam na Jack WarnerShirikisho la mchezo wa soka duniani Fifa, limewasimamisha kwa muda wajumbe wawili wa kamati kuu, Mohamed Bin Hammam na Jack Warner baada ya kikao cha kamati yake ya maadili siku ya Jumapili.
Shirikisho hilo sasa litaanzisha uchunguzi kamili juu ya madai kwamba wajumbe wa shirikisho la soka la Caribbean walipewa rushwa.
Maafisa wawili wa shirikisho hilo Debbie Minguell na Jason Sylvester pia wamesimamishwa.
Lakini rais wa Fifa Sepp Blatter hakupatikana na hatia yoyote.
Petrus Damaseb,makamu mwenyekiti wa kamati ya maadili, alisema haya juu ya Bin Hammam na Warner: "tumeridhika kwamba kuna majibu tunayohitaji kuhusu suala hili."
Hata hivyo, Fifa imesisitiza kuwa hawana hatia kwa sasa hadi itakapothibitishwa kuwa walihusika katika sakata hilo.
Kama watapatikana na hatia, wanaweza kufukuzwa kutoka shirikisho hilo na kupigwa marufuku kushiriki shughuli zozote za mpira wa miguu.
Bin Hammam alikuwa mpinzani pekee wa Blatter katika uchaguzi ujao wa urais wa Fifa lakini alijiondoa mapema siku ya Jumapili.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Wasifu wa Kizza Besigye

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA