HABARI ZA KUSIKITISHA


Na Mwandishi Wetu
MPIGAPICHA Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Richard Mwaikenda (pichani) ambaye pia ni mmiliki wa blogu hii ameporwa begi lenye kamera na kompyuta na vibaka waendesha pikipiki.
Vibaka hao waliokuwa wamepakizana kwenye pikipiki, walimpora begi hilo lililokuwa kiti cha mbele cha gari lake alilokuwa akiendesha likiwa karibu na makutano ya barabara za Kitunda na Nyerere, eneo la Banana, Ukonga, Dar es Salaam jana asubuhi.
Aliyechukua begi kwenye gari ni kibaka aliyepakizwa nyuma na pikipiki hiyo kuondoka kwa kasi kuelekea Ukonga na kumwia vigumu mpiga picha huyo kuachia usukani kuwafukuza kwani magari yalikuwa yameanza kutembea.
Alitaja vitu vingine vilivyokuwemo kwenye begi hilo kuwa ni, Modemu ya Vodacom, kifaa cha kutolea picha kutoka kamera ya digito kwenda katika kompyuta (Cardreader), Flash, vitambulisho vya kazi na nyaraka muhimu.
Akisimulia tukio hilo, Mwaikenda alisema , inaelekea vibaka hao walimfuatilia kutoka Kitunda ambapo alisimamisha gari lake na kuchukua kamera kwenye begi na kupiga picha mashimo makubwa barabarani karibu na Kituo Kidogo cha Polisi cha Kitunda.
Mwaikenda alikuwa anatokea nyumbani kwake, Kivule kwenda Pugu Kanisani kuripoti tukio la Ibada ya misa ya shukrani kwa Hayati Papa John Paul wa Pili kutangazwa Mwenye Heri.
Ibada hiyo iliongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Mwaikenda alisema alitarajia kutoa taarifa Polisi juu ya wizi huo wa kutumia pikipiki ambao umekithiri katika miji mbalimbali.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*