ICC YATAKA HATI YA KUKAMATWA GADDAFI

ICC yataka hati ya kukamatwa kwa Gaddafi
LibyaMwendesha mashtaka wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC inataka kutoa hati ya kukamatwa kwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi na wengine wawili kwa uhalifu dhidi ya binadamu.
Luis Moreno-Ocampo alisema Kanali Gaddafi, mtoto wake wa kiume Seif al-Islam, na mkuu wa idara ya ujasusi Abdullah al-Sanusi wamehusika kwa "mashambulio yaliyopangwa kwa ufanisi na kutapakaa" kwa raia.
Majaji wa ICC bado wanatakiwa kuamua iwapo watoe hati ya kukamatwa kwao au la.
Serikali ya Libya tayari imesema itapuuza hatua hiyo.
Naibu waziri wa mambo ya nje Khalid Kaim alisema mahakama hiyo ni "mtoto wa Umoja wa Ulaya ulioandaliwa kwa ajili ya wanasiasa na viongozi wa Afrika" na shughuli zake "zinatia shaka".
Alisema, Libya haikuitambua mahakama hiyo, kama ilivyo kwa nchi nyingi za Afrika na Marekani, na itapuuza tangazo lolote.


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*