IMF YASHINIKIZWA UTEUZI MPYA WA BOSS



Mkuu wa IMF Dominique Strauss-Kahn mahakamaniWaziri wa fedha wa Marekani amesema kuwa mkuu wa shirika la fedha duniani (IMF), Dominique Strauss-Kahn, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya kujaribu kumbaka mhudumu wa hoteli, hawezi tena kuendesha shughuli za shirika hilo.
Timothy Geithner ametoa wito kwa IMF kumteua rasmi kaimu mkuu wa shirika hilo.
Bwana Strauss-Kahn anazuiliwa katika jela moja mjini New York baada ya kukamatwa hapo jumamosi kwa kosa la kujaribu kumbaka mhudumu wa hoteli moja.
Strauss-kahn ambaye amezuiliwa katika gereza la wafungwa sugu la Rikers Islands mjini New York yupo chini ya ulinzi mkali kuchunga asijiue. Hii ni baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.
Wakili wa mwanamke huyo kutoka Guinea, Afrika Magharibi, anayemtuhumu Strauss-Kahn, amesema mteja wake amepata mshutuko ambao sio wakawaida.
Wakili huyo ameongeza kuwa kwa sasa yupo mafichoni na kwamba anajihisi ''Yuko pekee duniani''.
Strauss-Kahn, mwenye umri wa miaka 62, anakabiliwa na mashtaka saba dhidi yake na iwapo atapatikana na hatia, atahukumiwa kifungo cha hadi miaka 25 jela.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.