JK ATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA SHEIKH YAHYA HUSSEIN

Rais Jakaya Kikwete

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE KUFUATIA KIFO CHA SHEIKH YAHYA HUSSEIN

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Sheikh Yahya Hussein kufuatia kifo cha Mnajimu Mkuu huyo kilichotokea asubuhi ya leo tarehe 20 Mei, 2011, katika Hospitali ya Mount Ukombozi iliyoko Morocco Jijini Dar es Salaam.

“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Sheikh Yahya Hussein ambaye enzi za uhai wake alijipatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi kutokana na kipaji chake katika masuala ya unajimu wa nyota ambao ulimpatia sifa kubwa,” amesema Rais Kikwete katika rambirambi zake.

Ameongeza: “Naomba, kama familia, mpokee salamu zangu za pole kwa kuondokewa na kiongozi muhimu na tegemeo kubwa la familia. Namuomba Mwenyezi Mungu aiweke mahali pema peponi roho ya Marehemu. Amina.”

Amesema Rais Kikwete katika salamu zake: “Naelewa fika machungu mliyonayo katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wenu. Najua alikuwa mzazi, alikuwa baba, alikuwa babu, alikuwa mlezi na tegemeo kubwa la familia. Najua ameacha pengo kubwa ambalo litakuwa gumu kuzibika. Najua mko katika kipindi kigumu na cha majaribio. Hivyo nawaombeni muwe na moyo wa uvumilivu na subira. Yote ni mapenzi ya Mola. Napenda kuwahakikishieni kuwa niko nanyi katika kipindi hiki cha maombolezo ya msiba wa mpendwa wenu.”

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI