KAFULILA AKAGUA UJENZI WA BARABARA YA LAMI JIMBONI

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali mstaafu Joseph Simbakalia (aliyevaa suti nyeusi) pamoja na vingozi wengine wa mkoa huo akiwemo Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila wakiangalia eneo patakapojengwa daraja jipya la Mto Malagalasi, walipotembelea eneo hilo hivi karibuni.

Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila (kushoto) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali mstaafu, Joseph Simbakalia (katikati) walipokuwa wakipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Wakala wa Barabara wa Serikali (TANROADS), Mkoa wa Kigoma,Haruna Senkuku kuhusu ujenzi wa Barabara ya kwanza ya lami ya Kidahwe-Uvinza yenye urefu wa Km 76 inayojengwa Jimbo la Kigoma Kusini,mkoani Kigoma. Viongozi hao wawili walitembelea mradi huo mwishoni mwa wiki.




Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Nguruka,mkoani Kigoma mwishoni mwa wiki iliyopita, ambapo aliwaeleza wananchi kutoa ushirikiano kwa wajenzi wa barabara ya lami ya Malagalasi-Nguruka yenye urefu wa Km 48, sambamba na ujenzi wa daraja la kihistoria la Malagalasi lenye urefu wa mita 275.





Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini,kupitia NCCR-Mageuzi, David Kafulila (kulia),akipongezwa na Diwani wa Kata ya Itebula (NCCR-Mageuzi), Shukuru Chiza baada ya kuhutubia mkutano wa kuwashukuru wananchi waliompigia kura katika Kata hiyo. Katikati ni Mwenyekiti wa Jimbo, Venance Mwaka. Mkutano huo ulifanyika katika Kata hiyo mwishoni mwa wiki.








Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini,kupitia NCCR-Mageuzi, David Kafulila (kushoto), akipongezwa na mmoja wa akina mama wakazi wa jimbo hilo, ambao watoto wao wamebahatika kusomeshwa na mbunge huyo ambaye ameanzisha mfuko maalum wa kuwasomesha watoto wasiopungua 300 kwa gharama ya milioni 60 ndani ya miaka mitano.Tukio hilo lilitokea baada ya mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wapiga kura kwa ushindi alioupata uliofanyika katika Kata ya Itebula.







Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA