Wanafunzi wa Chuo cha Sanaa Bagamoyo (TASuBA) wakiwasilisha ujumbe unaopiga vita matumizi ya bidhaa za tumbaku wakati wa maadhimisho ya Siku ya kutotumia tumbaku Duniani leo wilayani Bagamoyo.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hadji Mponda akizungumza na wananchi wa wilaya ya Bagamoyo leo wakati wa maadhimisho ya Siku ya kutotumia Tumbaku duniani ambayo kitaifa yamefanyika katika viwanja vya shule ya msingi Majengo Bagamoyo. Pamoja na mambo mengine amesema serikali imeandaa mpango mkakati wa miaka 5 kwa lengo la kudhibiti matumizi bidhaa za tumbaku nchini.
Comments