MABOMU YAUA WATU 10 NIGERIA




Karibu watu 10 wameuawa na wengine 20 kujeruhiwa baada ya bomu kulipuka karibu na kambi ya jeshi Kaskazini mwa Nigeria,maafisa katika eneo hilo wamesema.
Mlipuko huo ulitokea katika soko la Mamy mjini Bauchi siku ya Jumapili.
Watu waliojeruhiwa walipelekwa hospitalini.
Kufikia sasa hakuna kundi lililojitokeza kudai kuhusika na shambulio hilo.
Shambulio limetokea saa chache baada ya Goodluck Jonathan kuapishwa kwa muhula mpya wa miaka minne kama rais katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja.
Mlipuko mwingine ulitokea katika klabu cha pombe viungani mwa mji wa Abuja na kusababisha majeraha madogo, maafisa wanasema.
Goodluck JonathanSababu ya mlipuko huo haikuweza kufahamika mara moja.
Taarifa zingine zinasema kuwa kumekuwepo na milipuko mitatu katika muda mchache.
"kulikuwa na watu wengi kwa kuwa ni Jumapili jioni. Watu walikuwa wanaburudika,wanakula na kunywa," Kamishna wa polisi wa jimbo la Bauchi Abdulkadir Indabawa alinukuliwa na shirika la habari la AFP akisema.
Kambi za jeshi nchini Nigeria mara nyingine zinakuwa na sehemu ya soko ambako wafanyabiashara wanauza vyakula,vinywaji na bidhaa zengine kwa wanajeshi na raia.
Barabara za kuelekea kwenye kambi za kijeshi zilifungwa na maafisa wa usalama.


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.