MAJAMBAZI YATEKA MAGARI KITONGA

Tumaini Msowoya, IringaWATU kumi wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, wameteka magari mawili ya mizigo na kuwapora abiria waliokuwa wakisafiri kwa kutumia magari hayo, katika eneo la Mlima Kitonga, mkoani Iringa.Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Evarist Mangala, alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana baada ya watu hao kutega magogo barabarani na kusababisha magari hayo, kushindwa kupita.
Alisema magari hayo yaliyotekwa ni scania moja na Fuso na kwamba yote yalikuwa wanatokea jijini Dar es salaam, kwenda Iringa.Mangala alisema hata hivyo watu hao hawakuwa na bunduki na badala yake walikuwa fimbo, lakini idadi yao kubwa iliwawezesha, kuwateka abiria na baadaye, kukimbilia porini
Kamanda huyo alitaja vitu ambavyo majambazo hayo yalipora kutoka kwa abiria kuwa ni pamoja simu na mizigo mengine.“Polisi walipata taarifa na baadaye kwenda katika eneo la tukio ambako hata hivyo waliwakuta abiria wote wakiwa salama. Hii inaonyesha kuwa majambazi hayo, hayakuwa na silaha zaidi ya fimbo tu,” alisema Mangala.
Aliwataka wananchi, kutoa taarifa zitakazowezesha kukamatwa kwa watu hao na kufikishwa katika vyombo vya sheria.Alisema, polisi kwa upande wao, wameamua kuanza doria katika maeneo yote hatari likiwamo la Mlima Nyang’oro katika Barabara ya Iringa-Dodoma ambako pia kumekuwa na matukio ya aina hiyo.
“Tumeamua kuanza doria kwenye maeneo haya hatari kama Kitonga na kwingineko, lakini peke yetu hatutaweza kwa hiyo tunahitaji ushirikiano wa jamii," alisema.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.