MAPIGANO YASITISHWE LIBYA



Mapigano yasitishwe kwa muda Libya
Waasi mjini Misrata, LibyaMkuu wa idara ya kutoa misaada wa Umoja wa Mataifa Valerie Amos ametoa wito wa kusitishwa kwa muda mashambulio yanayofanywa Libya ili kupunguza mgogoro wa kibinadamu unaoendelea nchini humo.
Baroness Amos aliliambia baraza la usalama la umoja wa mataifa kwamba Misrata, ngome pekee inayoshikiliwa na waasi magharibi mwa Libya, iko katika hali mbaya na inakabiliwa na upungufu wa chakula pamoja na maji.
Takriban watu 750,000 wameikimbia Libya tangu ghasia kuibuka dhidi ya uongozi wa Kanali Muammar Gaddafi.
Wakati huo huo, majeshi ya umoja wa nchi za kujihami za Ulaya, Nato yamefanya mashambulio kwenye mji mkuu Tripoli, ikiwa ni harakati kali kufanyika katika wiki kadhaa zilizopita.
Ripoti zinasema majengo manne yalilengwa, likiwemo eneo la familia ya Kanali Gaddafi, shirika la kijeshi la kijasusi na makao makuu ya kituo cha televisheni ya taifa.
Serikali ilisema ofisi ya tume ya watoto nchini humo ilishambuliwa, na watoto wanne walijeruhiwa.
Imekuwa vigumu kuthibitisha taarifa hizo.
Huko Misrata, waasi wanasema wamefanikiwa kusogeza majeshi ya serikali.
Mji huo umezingirwa na majeshi yanayomtii Kanali Gaddafi kwa miezi miwili sasa.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.