MBEYA USO KWA USO NA MWANZA FAINALI





TIMU ya soka ya mkoa wa Mbeya, jana iliifuata Mwanza kwenye fainali ya Kili Taifa Cup baada ya kuibamiza Kagera - Lweru Eagles- mabao 2-1 katika mchezo wa nusu fainali iliyopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini hapa.

Mbeya imekwenda fainali hizo kupitia kwa mabao yaliyowekwa kimiani na Gaudence Mwaikimba (pichani kulia) na lile la kujifunga la Luhende Charles katika dakika ya 93 baada ya kumalizika zile 90 za kawaida kwa sare ya 1-1.

Bao la Mwaikimba lililopatikana kwa penati baada ya kipa wa Kagera kumwangusha Said Mtupa na mshambuliaji huyo mrefu hakufanya ajizi kufunga na Themi Felix alilifuta kwenye dakika ya 60 kutokana na walinzi wa Mbeya kushindwa kuondosha hatari hiyo.

Kutokana na ushindi huo, sasa Mwanza kutoka Green City wataivaa Mwanza kutoka Rocky City katika fainali ambayo inatarajiwa kuwa kali na ya kuvutia itakayopigwa Jumamosi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.