MBINU MPYA YA KUPAMBANA NA UHARAMIA

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na safari za meli duniani, IMO, kwa mara ya kwanza limetoa idhini kwa makampuni ya ulinzi ya kibinafsi, kuzikinga meli na uharamia.

Baada ya kukutana kwa siku tisa mjini London, IMO imetoa mwongozo kuhusu namna makampuni na walinzi binafsi wenye silaha, wanavoweza kuendesha shughuli zao ndani ya meli katika maeneo ya hatari, pamoja na kando ya mwambao wa Somalia.
Asili mia 10 ya meli katika eneo hilo zinakuwa na walinzi wao binafsi wenye silaha, lakini wadadisi wanasema idadi hiyo inaweza kuzidi baada ya Umoja wa Mataifa kutoa idhini.
Msemaji wa IMO, Peter Cook, ameiambia BBC kuwa ulinzi unaotolewa na manuwari za kimataifa hautoshi:
"Majeshi ya wanamaji ya kimataifa hayawezi kutoa ulinzi wa kutosha kwa sababu hayana tena vifaa.
Kwa hivo ni wazi kuwa lazima ichukuliwe hatua ili kufanya biashara huru iendelee.
Kwa sababu hivi sasa, imefika hadi kuwa uharamia unaanza kutishia bidhaa kupita katika Bahari ya Hindi na Mfereji wa Suez."

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.