MKE WA MUBARAK ATIWA KIZUZINI KWA UFISADI



Mke wa rais aliyeondolewa madarakani nchini Misri, Hosni Mubarak amezuiwa kwa siku 15 kwa ajili ya uchunguzi wa tuhuma za rushwa, limeripoti shirika la habari la taifa hilo.
Suzanne Mubarak
Suzanne Mubarak atazuiliwa katika gereza moja mjini Cairo, shirika la habari la Mena limesema.
Bi Mubarak, 70, na mume wake wamehojiwa kuhusiana na tuhuma za "upataji mali kinyume cha sheria".
Rais Mubarak, ambaye alikaa madarakani kwa miaka 30, aliondoka madarakani mwezi Februari baada ya wiki kadhaa za maandamano.
Rais huyo wa zamani anashikiliwa na mamlaka za nchi hiyo zinazohusiana ma upatikanaji wa mali kintyume cha sheria, kwa mashitaka ya kutumia vibaya madaraka yake na kujipatia utajiri. Pia anatuhumiwa kwa kuhusika na mauaji ya watu waliokuwa wakipinga utawala wake.
Bw Mubarak, 80, kwa sasa yuko hospitali katika mji uliopo kwenye mwambao wa bahari ya Sham wa Sharm el-Sheikh, baada ya kupata matatizo ya moyo.
Baraza la kijeshi ambalo limeingia madarakani tangu Bw Mubarak aondoke, limeahidi kuwafikisha mahakamani wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU