MKUTANO WA MAKOCHA, MAREFA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litakuwa na mkutano na makocha na waamuzi wote wa mpira wa miguu wanaoishi Dar es Salaam. Marefa na makocha wanaotakiwa kuhudhuria mkutano huo ni wa madaraja na ngazi zote. Mkutano huo utafanyika Jumamosi (Mei 28 mwaka huu) kwenye ofisi za TFF zilizoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume wilayani Ilala kuanzia saa 3.30 asubuhi. Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Sunday Kayuni ndiye atakayekuwa mzungumzaji mkuu katika mkutano huo. Tunawaomba makocha na marefa wote wanaoishi au walioko Dar es Salaam kuhudhuria mkutano huo muhimu kwa maendeleo ya mpira wa miguu katika Mkoa wa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla. Boniface WamburaOfisa Habari TFF

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA