MLEVI MBARONI KWA KUWAPIGIA POLISI KUWA AMEISH IWA KILAJI

Polisi nchini Marekani wamemkamata na kumshitaki bwana mmoja kwa kutumia vibaya namba ya simu ya dharura
Mtandao wa cnews.com umesema polisi walimshitaki Bwana Raymond Roberge mwenye umri wa miaka 65, kwa kupiga simu hiyo, namba 911.
Bwana huyo alipiga simu hiyo na kusema amepatwa na dharura, na alipoulizwa dharura gani, alijibu kuwa ameishiwa bia alizokuwa anakunywa. Taarifa zinasema bwana huyo wa mjini Bridgeport, Connecticut, alipiga simu mara tatu, akiomba kutatuliwa dharura yake hiyo.
Gazeti la Connecticut Post pia limeripoti kuwa hii si mara ya kwanza kwa Bwana Raymond kufanya hivyo, kwani amekwishawahi kupiga simu huyo pasipo na dharura rasmi, takriban mara themanini.


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.