MUBARAK NA WANAWE WASHITAKIWA

Mtoto wa Mubarak, Gamal

Aliyekuwa rais wa Misri Hosni Mubarak na watoto wake wawili wa kiume wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakituhumiwa kwa kosa la mauaji na ufujaji wa mali ya umma.
Wote watatu wameshikiliwa huku watoto wakiwa gerezani na Bw Mubarak akiwa hospitalini huko Sharm el-Sheikh.
Mwendesha mashtaka mkuu wa Misri alitangaza Hosni Mubarak na watoto wake wa kiume Gamal na Alaa wanatarajiwa kushtakiwa kwa mauaji na rushwa.
Wanashutumiwa kwa kupanga mauaji ya waandamanaji katika mapinduzi yaliyoanza Januari 25.
Lengo lao kulingana na shutuma hizo ni kuua baadhi na kuwatisha wengine.
Aliyekuwa rais anatuhumiwa kwa kukubali kupokea zawadi, ikiwemo kasri na nyumba za kifahari nne katika eneo la Sharm el-Sheikh.
Bw Mubarak pia anatuhumiwa kufanya njama na mfanyabiashara, ambaye anashtakiwa naye, kwa kuuza gesi kwa bei rahisi huko Israel hivyo kufanya udanganyifu wa mamilioni ya dola dhidi ya serikali ya Misri.
Kulingana na ripoti moja, kundi la madaktari kwa sasa limeenda kumtemebelea Bw Mubarak hospitalini Sharm el-Sheikh na kutathmini iwapo ana uwezo wa kusafiri kwenda Cairo, aidha apelekwe hospitali kwenye mji mkuu au gerezani walipo tayari wanawe wawili.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*