MUSEVENI KUAPISHWA LEO

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni,anatarajiwa kuapishwa kwa muhula mwengine hii leo siku ya Alhamisi.Anaapishwa huku kukiwa na wingu la shutma kwa utawala wake kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya upinzani.
Katika siku za hivi karibuni serikali imelaumiwa kwa namna walivyokabiliana na maandamano ya upinzani na kusababishwa kulazwa hospitali kwa mwanasiasa wa upinzani, Dk Kizza Besigye pia kumezua shutma kali.
Wakati atakapoapishwa kwa muhula mwengine,Yoweri Museveni atakuwa amejiongezea muda wa kukaa madarakani kwa takriban miaka thelathini.
Alipoingia madarakani mwaka 1986 alisema tatizo la viongozi wa Afrika ni kukaa kwenye utawala kwa muda mrefu sana.
Kwa miaka mingi amefanya juhudi kuijenga upya nchi ya Uganda baada ya nchi hio kuwa kwenye vita na utawala mbaya.
Bado anaungwa mkono na wengi lakini wadadisi wanaona kuendelea kutegemea jeshi kunaweka nchi hio katika mazingira magumu.
Kizza Besigye akikabiliana na polisiUpinzani umekabiliwa vibaya katika wiki za hivi karibuni. Kiongozi wa upinzani, Dokta Kizza Besigye,bado yuko nchini Kenya baada ya kupata matibabu kufwatia kushambulia kwake na polisi.
Mapema siku ya Jumatano,Besigye alisema kuwa alizuiwa kupanda ndege kutoka Nairobi kwenda Uganda, baada ya kupatiwa matibabu nchini Kenya.
Serikali ya Uganda imekanusha kumzuia kusafiri.
Haijulikani kama atajaribu kusafiri hii leo kwenda nyumbani wakati Rais Museveni anaapishwa - hatua ambayo italeta aibu kwa serikali.
Baadhi ya viongozi walioalikwa kwa sherehe za kuapishwa kwa Rais Museveni waliwasili Kampala siku ya Jumatano huku wengine wakitarajiwa hii leo siku ya Alhamisi

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*