NSSF YAWAKUNA WAJASIRIAMALI DAR

Ofisa Uhusiano wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mwanakombo Mohamed akigawa mfuko wenye fulana, kofia na vijarida vya NSSF kwa wanachama wa kikundi cha wajasiriamali cha akina mama wa Ubungo cha MUWASIDA Saccos, waliohudhuria semina ya elimu ya umma kuhusu mfuko huo, Dar es Salaam









Mwanachama wa kikundi cha wajasiliamali cha akina mama wa Ubungo cha MUWASIDA Saccos, Editha Rimoy akisoma kijarida cha mafao ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), alichopewa wakati wa semina ya elimu ya umma kuhusu mfuko huo, Dar es Salaam juzi.










Mwanachama Hidaya Mohamed wa kikundi cha wajasiriamali cha akina mama wa Ubungo cha MUWASIDA Saccos, akiuliza swali kwa mwendesha mada, Chritene Kamuzora (kutoka) kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), wakati wa semina ya elimu ya umma kuhusu mfuko huo, Dar es Salaam juzi.








Ofisa Matekelezo Mwandamizi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Chritine Kamuzora (kulia), akielezea faida ya kujiunga na mfuko huo katika semina ya elimu ya umma kuhusu mfuko huo, iliyowahusisha wanachama wa kikundi cha wajasiliamali cha akina mama wa Ubungo cha MUWASIDA Saccos, Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Ofisa Uhusiano wa NSSF, Maife Kapinda.
















Ofisa Matekelezo Mwandamizi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Chritine Kamuzora (kulia), akielezea faida ya kujiunga na mfuko huo katika semina ya elimu ya umma kuhusu mfuko huo, iliyowahusisha wanachama wa kikundi cha wajasiliamali cha akina mama wa Ubungo cha MUWASIDA Saccos, Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Ofisa Uhusiano wa NSSF, Maife Kapinda.




Na Mwandishi Wetu

WAJASIRIAMALI wamekunwa na mpango wa Mfuko wa

Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), wa kuwapatia

mafao ya mishahara ya miezi mitatu
Wanawake wanachama wao wanaojifungua.

Wajasiriamali wa Kikundi cha Muungano wa

Wanawake wa Sekta isiyo rasmi Dar es Salaam

(MUWASIDA SACCOS) waliufurahia mpango huo

ulioelezwa, Dar es Salaam juzi, na Ofisa

Matekelezo Mwandamizi wa NSSF, Christine Kamuzora

katika semina ya siku moja ya elimu ya umma

kuhusu faida lukuki anazoweza kuzipata mwanachama

wa mfuko huo.

Alisema kuwa licha ya Mwanamke mjamzito kupata

mafao lakini vile vile hunufaika zaidi kwa NNS

kumpatia jumla ya mishahara miezi mitatu

anapojifungua ili imsaidie wakati wa kulea mtoto.

Kamuzora alisema kiwango cha mshahara kinatolewa

kulingana ama zaidi ya mshahara unaotolewa na

mwajiri wa mwanachama huyo.

Alisema, mpango maalumu unaandaliwa kwa

wajasiriamali wa kujitolea ambao si wafanyakazi

ili nao wanufaike na mpango huo pamoja na mafao

mengine yatolewayo na mfuko huo.

Pia Kamuzora, alitumia fursa hiyo kuwaeleza

wajasiriamali hao, kuhusu umuhimu wa kujiunga na

mfuko huo ili wanufaike na mafao mbalimbali

yanayotolewa kwa wanachama.

Alitaja mafao hayo kuwa ni; Pensheni ya uzeeni,

Pensheni ya Ulemavu, Pensheni ya Urithi,mafao ya

Matibabu,Mafao ya Uzazi,Mafao ya Kuumia Kazini na

Mafao ya Mazishi.

Aliwaeleza kuwa katika Mafao ya Matibabu

wanachama wajasriamali hunufaika kwa kupatiwa

huduma ya tiba bure kwa miezi mitatu hata akiacha

kuchangia mfuko ambao ni asilimia 20 ya mshahara

ama kipato anachopata katika biashara zake.Lakini

kwa wafanyakazi waliochangia muda mrefu hunufaika

kwa kupatiwa tiba bure hadi kifo chake.

Alisema huduma hiyo ambayo hupatikana katika

hospitali walizoingia nazo mkataba, hutolewa bila

ubaguzi kwani kila mwanachama ana haki hiyo na

kwamba hawana madaraja ya juu, kati wala ya

chini.Wanaonufaika katika mpango huo kifamilia ni

Baba, Mama na Watoto wanne.


Kamuzora alitoa mwito kwa wajasiriamali kujiunga

kwa wingi ili wanufaike na mafao hayo na

kusisitiza kuwa wasiwe na hofu yoyote kwani NSSF

imesimama imara hata vitukuu vyao wataikuta,

haitetereki kwa upepo, kimbunga wala Tsunami.







Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI