NYOTA WA NJE WAMIMINIKA TAIFA STARS


SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF) limetangaza utaratibu wa
wachezaji wanaocheza soka la kulipwa ughaibuni watakavyouungana na wenzao kabla ya kucheza na Jamhuri ya Afrika ya Kati (RCA) katika mechi ya kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika.

Katibu Mkuu wa TFF Angetile Osiah alisema kuwa tayari wamefanya mawasiliano na wachezaji saba wanaocheza njena wana uhakika wa kuwapata kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa mjini Banjui, RCA.

Alisema kuwa Nizar Khalfan anayekipiga klabu ya Whitecaps ya Canada anatarajia kujiunga na wenzake Juni 2, Idrissa Rajab ambaye anakipiga Sofapaka ya Kenya ataungana na wenzake Juni 2, siku moja tu baada ya kucheza mechi ya Kombe la
Shirikisho mjini Tunis, Tunisia.

Osiah alisema kuwa Henry Joseph anayechezea klabu ya Kongsvinger IF ya Norway na Athuman Machupa anayekipiga Vasalunds ya Sweden watakuwepo nchini kesho. Abdi Kassim na Danny Mrwanda wanaochezea timu ya DT Long An ya Vietnam.

Pia katibu huyo alisema kuwa shirikisho lake limepeleka ombi kwa klabu ya TP Mazembe ili iweze kumruhusu Mbwana Samatta ili kuungana na wenzake walio kwenye timu ya taifa.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI