Rais Goodluck Jonathan aapishwa Nigeria


Viongozi wa Afrika na maelfu ya watu maarufu walihudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan (pichani), katika medani ya mji mkuu, Abuja

Sherehe zilianza kwa wimbo wa taifa na kulikuwa na ulinzi wa hali ya juu.

Maombi yaliendeshwa na wakuu wa dini za Kiislamu na Kikristo nchini humo.

Uchaguzi uliofanyika mwezi uliopita ulikumbwa na vifo vya mamia ya raia, katika ghasia zilizoibuka, ingawaje wengi wanasema uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki.

Bw Jonathan alishika hatamu ya uongozi baada ya Umaru Yar-Adua kufariki dunia takriban mwaka moja uliopita.

Rais Jonathan, maarufu kwa kofia yake kubwa, na kuupenda mtandao wa intaneti wa facebook, ameorodhesha majukumu mengi ya kutimiza, na wengi wataona amejipa kibarua kigumu, kama ataweza kuyatekeleza.

Muhimu zaidi ni kurejesha huduma ya umeme, na kuondosha rushwa.

Uchaguzi huo ulileta wasiwasi baina ya pande za kaskazini na kusini mwa Nigeria.

Rais Goodluck Jonathan anakabiliwa na jukumu la kuonesha kuwa hana mapendeleo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA