TALIBAN INASHAMBULIA VIKALI KANDAHAR

Taliban inashambulia vikali KandaharShughuli zimesimama katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Afghanistan, mji wa Kandahar, kusini mwa nchi, kwa sababu ya mapigano makali, yaliyozushwa na mashambulio kadha yanayofikiriwa kufanywa na wapiganaji wa Taliban dhidi ya majengo ya serikali.

Mashambulio kama sita yamefanywa na watu waliojitolea mhanga.
Mapigano mengi yametokea kwenye maeneo ya biashara.
Watu wengi walijeruhiwa.
Rais wa Afghanistan, Hamid Karzai, alisema Taliban wanajaribu kuficha kuwa wameshindwa kwa Osama Bin Laden kuuwawa, kwa kulipiza kisasi kwa kushambulia raia wasiokuwa na hatia.
Taliban imekanusha kuwa mashambulio hayo ni ya kujibu mauaji ya Bin Laden, na wamesema mashambulio hayo yalipangwa kitambo.


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*