TFF YAAJIRI KOCHA WA TIMU ZA VIJANA

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemwajiri Kim Poulsen, raia wa Denmark kuwa kocha wa timu za Taifa za vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) na chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) kuanzia Mei 15 mwaka huu. Poulsen mwenye leseni ya kulipwa ya ukocha ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA) katika ngazi ya diploma, na mkufunzi wa makocha wa kiwango cha juu anayetambuliwa na Chama cha Mpira wa Miguu Denmark (DBU) amesaini mkataba wa miaka miwili. Kabla ya kujiunga na TFF, Poulsen alikuwa kocha wa timu ya FC Hjorring inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Denmark kuanzia Julai mwaka jana hadi Mei Mosi mwaka huu. Mwaka 1989 alikuwa kocha bora wa mwaka nchini Denmark. Tuzo hiyo pia aliipata mwaka 2004 na 2005 nchini Singapore ambapo alikuwa kocha wa timu ya Taifa chini ya umri wa miaka 23. Mwaka 2002 hadi 2003 alikuwa kocha wa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 18 ya Singapore. Mbali ya sifa za ukocha, uteuzi wake pia umezingatia utaratibu wa TFF wa kuwa na makocha wenye falsafa moja ya mpira, hali ambayo inawajengea misingi mizuri wachezaji wa timu za vijana wanaopata fursa ya kuchezea timu ya wakubwa (Taifa Stars).
Utaratibu huo tuliuanzisha toka wakati wa Marcio Maximo akiinoa Stars ambapo makocha wa vijana nao walikuwa wakitoka Brazil. Kocha wa sasa wa Taifa Stars, Jan Poulsen naye anatoka Denmark, na hana uhusiano wowote wa damu na Kim.
Boniface WamburaOfisa Habari TFF

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA