UHALALI WA WACHEZAJI SAMATA, OCHAN

Wachezaji Mbwana Samata na Patrick Ochan ambao Simba inataka kuwatumia kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco hawana uhalali wa kuchezea timu hiyo. Simba kupitia TFF ilitaka kufahamu kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kama inaweza kuwatumia wachezaji hao kwa vile Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kuichezea TP Mazembe bado haijatolewa. Kwa mujibu wa CAF, hawawezi kuichezea Simba kwa vile tayari wameuzwa, hivyo kutokuwa na sifa ya kuwa wachezaji wa timu hiyo kwa mujibu wa Ibara ya 26(1) ya Kanuni za Ligi ya Mabingwa Afrika.
Sifa ya mchezaji kwa mujibu wa kanuni hiyo ni kuwa na leseni iliyotolewa na chama cha mpira wa miguu cha nchi yake, leseni ya CAF, awe anaichezea timu inayoshiriki Ligi ya Mabingwa kwenye ligi ya nchi husika na awe anaishi katika nchi ilipo timu anayoichezea.
U 23 v NIGERIA- MICHUANO YA OLIMPIKIMechi ya kwanza ya mchujo ya michuano ya Olimpiki kati ya timu ya Taifa ya Tanzania kwa vijana wenye umri chini ya miaka 23 dhidi ya Nigeria itachezwa Juni 5 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 1 kamili usiku.
Tumepanga muda huo kwa vile uwanja siku hiyo utakuwa unatumika kwa ajili ya michuano ya riadha ya Kanda ya Tano Afrika ambapo itakuwa inafikia kilele. Kwa mujibu wa Chama cha Riadha Tanzania (AT) kufikia saa 8 mchana michuano hiyo itakuwa imemalizika, hivyo kupisha maandalizi ya mechi. Mechi itachezeshwa na mwamuzi Sylvester Kirwa ambapo atasaidiwa na Peter Kiereini, Aden Marwa na Davies Omweno wote kutoka Kenya wakati Kamishna wa mchezo huo atakuwa Sahilu Gebremariam kutoka Ethiopia. Boniface WamburaOfisa Habari TFF

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA