UN yaamrisha jeshi la Sudan kuondoka Abyei

Moto ukiwaka katika mji wa AbyeiBaraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeitaka jeshi la utawala wa Khartoum nchini Sudan kuondoka katika jimbo la Abyei.
Jeshi hilo lilitwaa mji wa Abyei hapo Jumamosi ambapo majeshi ya utawala wa Kusini yaliondoka baada ya mapigano makali.
Shambulizi hili limetokea wakati Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekuwa ziarani Sudan. Baraza hilo limelaani mapigano hayo ya Abyei.
Mjumbe maalum wa Marekani nchini Sudan Pricenton Lyman amesema kitendo cha jeshi la Kharoum ni hatari kwa usalama wa taifa.
Nyumba zilizoharibiwa AbyeiKwa upande wake Serikali ya Sudan kusini imesema kutwaaliwa na jimbo la Abyei ni tangazo la vita. Barnaba Marial waziri wa mawasiliano Sudan Kusini amelaumu Khartoum kwa kutatua matatizo yake kwa kutumia vujo.
Shirika la kutoa misaada la MSF limesema zaidi ya watu elfu 20 wamekimbia mwakao.
Kwa sasa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linatarajia kufanya ziara rasmi kusini mwa nchi ambapo litazuru maeneo ya Wau na Juba.
mapigano ya Abyei yamezidisha taharuki wakati Sudan Kusini ikijitayarisha kujitenga na kaskazini katika miezi michache ijayo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.