UVCCM ARUSHA YATOA TAMKO KALI

TAMKO LA VIJANA WA CCM MKOA WA ARUSHA
Tarehe 25/05/2011Ndugu zangu waandishi wa habari leo tumeona tuwaite hapa ili tuwezekutoa maoni yetu kuhusiana na mustakabali wa chama chetu cha Mapinduzina Jumuiya yetu ya Umoja wa vijana wa CCM mkoa wa Arusha.Tumewaita hapa kwa malengo makuu Sita:-Kuunga mkono Halimashauri kuu ya CCM Taifa kwa kuona umuhimu wakuifanyia kazi kwa vitendo falsafa ya kujivua gamba. Tunaipongeza nakuiunga mkono Halmashauri kuu ya CCM Taifa kwa kutambua kwambamafisadi wamechangia sana kukidhoofisha na kukipotezea mvuto chamachetu mbele ya umma wa watanzania. Kwa mantiki hiyo tunatamka kwakauli moja kwamba mapacha hao watatu wa kifisadi ambao ni EdwardLowasa, Rostam Azizi na Andrew Chenge na vibaraka wao wafukuzwe maramoja kwa maslahi ya CCM na Watanzania. Pia tunasisitiza kuwa AndrewChenge aondolewe kwenye kamati ya maadili ya CCM mara moja na wakatihuohuo Edward afukuzwe kwenye kwenye ya uwenyekiti wa Bodi ya udhaminiya umoja wa vijana wa CCM Taifa haraka iwezekanavyo.Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arushatunamtaka kuwa James Millya ambaye ni kibaraka mkuu wa mafisadi mkoawa Arusha ajiuzulu mara moja na tunatamka rasmi kumfukuza kwenye UVCCMmkoa wa Arusha ili apate fursa ya kwenda kuwa tumikia mafisadi.Tunamtaka James Millya aache kufikiria kwa kutumia tumbo na badalayake atumie kichwa. Pia tumeshaandika barua yenye kumbukumbu nambakumb. Ars/Malalamiko/01 kwenye Chama kuelezea namna alivyo mnafiki,mfitini,mwongo na namna asivyo jali maslahi ya vijana wa UVCCM mkoa waArusha. Vilevile tunapenda kuujulisha umma wa Tanzania kuwa AllyBananga anaetumiwa na Millya pamoja na mafisadi hana nafasi yoyotendani ya Umoja wa vijana wa CCM kuanzia kwenye tawi hadi Taifa. Kwamantiki hiyo Ally Bananga aache mara moja kuganga njaa kwa kutumiajina la UVCCM. Pia tunampa onyo kali Catherine Magige aache mara mojakutumia fedha za mafisadi kuwagawa vijana wa Arusha kabla hatujatumiahaki yetu ya kikanuni ya kumsimamisha Ubunge. Tunajua kuwa amepataubunge kwa nguvu za kifisadi kupitia UVCCM.Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arushatunakiomba chama cha cha mapinduzi kiwafukuze mara moja makatibu waUVCCM kutoka wilaya za Monduli, Arumeru, Longido na Karatu kwakushiriki mandalizi ya maandamo haramu na kwa kukataa wito wa chama wakwenda kutoa ushahidi wa malamiko yao kuhusu mjumbe wa Baraza kuu laUVCCM Taifa. Kitendo hicho cha kukataa wito wa Chama ni dharau naukosefu wa maadili.Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arushatunatamka kwamba ili kulinda hadhi ya CCM mkoa wa Arusha tunamtakaOnesmo Nangole ajiuzulu mara moja kwa kuwa anafanya kazi ya FisadiEdward Lowasa na si ya CCM. Kitendo chake yeye cha kufanya kazi yamafisadi na si ya CCM kimetupelekea kupoteza majimbo mawili kwenyeuchaguzi mkuu wa 2010.Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arushatunatamka kwamba Mhe. Mary Chatanda (MB) ambaye ni katibu wa CCM Mkoawa Arusha ni mpiganaji na ni lulu ya CCM mkoa wa Arusha. Amefanyamengi ya maana na wa-CCM makini, wazalendo na wanaojali maslahi yachama chetu wanatambua hilo. Pia tunawaomba CCM Taifa waendeleekumwacha hapa Arusha ili aendelee kukijenga chama na kukomeshamafisadi pamoja na dagaa wao.Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arushatunatamka rasmi kumtambua Ndugu. Mrisho Gambo kuwa ni mjumbe halali wabaraza kuu la UVCCM Taifa kuwakilisha mkoa wa Arusha. Tunamuunga mkonokwa ujasiri wake, umahiri wake na uzalendo wake wa kupambana naufisadi ndani ya chama na Tanzania kwa ujumla. Na huo ndiyo msimamowetu kwa kuwa una tija kwa vijana wa Tanzania. Tunashauri CCM Taifakuwaita rasmi mapacha watatu wa kifisadi (Edward Lowasa, Rostam Azizina Andrew Chenge) kwenye kamati ya maadili ya CCM Taifa na kishakuwafukuza mara moja kama kweli tuna nia ya kuendelea kuwa chamatawala katika nchi hii.
TUTASEMA KWELI DAIMA FITINA KWETU MWIKOKAULI YETU: KULINDA NA KUJENGA UJAMAAKITADUMU CHAMA CHA MAPINDUZI BILA MAFISADI

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*