WAASI WASHAMBULIA KAMBI YA JESHI PAKISTAN

Makamanda wa Jeshi la Pakistan

Mwanajeshi aliyejeruhiwa
Takriban watu 11 wameuawa na wanamgambo katika shambulizi la mabomu na bunduki lililolenga katika kambi ya jeshi mjini Karachi, Pakistan.
Mmoja wa waliouawa ni afisa wa kijeshi mwenye uraia wa kigeni.
Maafisa wamesema zaidi ya wanamgambo kumi walihusika kwenye shambulio hilo.
Shambulio hili ni la tatu kulenga kambi hiyo tangu Aprili 26.
Kundi la Taleban tawi la Pakistan limekiri kuhusika na mashambulio ya hapo awali.
Miale ya moto imekuwa ikionekana kwa umbali huku milio ya risasi ikisikika kati ya wanajeshi na wanamgambo walioingia kambini hiyo.
Maafisa wa usalama wameambia BBC kwamba wanamgambo kadhaa walivamia kambi ya jeshi yenye ulinzi mkali kati kati mwa Karachi.
Walioshuhudia wamesema wanamgambo walitumia makombora kuharibu ndege za kivita zinazomilikiwa na jeshi la Pakistan.
Viongozi wa Kijeshi nchini PakistanBaadaye wanamgambo walianza kufyatua risasi hewani kiholela na kuwaua maafisa kadhaa wa kijeshi.
Katika kujibu mashambulio majeshi yalijaribu kuwafyatuliwa risasi wanamgambo hao.
Kufikia sasa majeshi zaidi yametumwa katika kituo hicho ambapo yameweza kuingia na kukabiliana na wapiganaji.
Baadhi ya wanamgambo wamewateka maafisa wa kijeshi ndani ya majengo ya kambi hiyo.
Shambulio la kambi ya Mehran ndilo la karibuni kufuatia mauaji ya kiongozi wa mtandao wa Al Qaeda Osama Bin Laden.



Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA