WASIFU WA OSAMA

Osama bin Laden

WASIFU WA OSAMA BIN LADENOsama bin Laden alizaliwa mwaka wa 1957, katika familia ya kitajiri nchini Saudi Arabia
Ana zaidi ya ndugu na dada 50. Babayake Osama alimiliki kampuni kubwa ya ujenzi. Katika baadhi ya picha zake za utotoni, Osama ameonyeshwa akiwa amevalia mavazi ya kifahari na ya gharama kubwa, akiwa likizo katika miji mbali mbali barani Ulaya.
Hata hivyo mwanzoni mwa miaka ya themanini alitapa mgongo maisha haya ya kifahari na kitajiri na kujiunga na vuguvugu la kupigania haki dhidi ya utawala wa Kisovieti baada ya majeshi yake kuishambulia Afghanistan.
Wakati huo, akipigana pamoja na Waarabu wenzake, alizindua kundi la kigaidi la Al Qaeda. Mnamo mwaka wa 1998, alitangaza fatwa yaani vita vikali vya kidini dhidi ya Marekani. Osama alisema alikasirishwa na hatua ya Marekani kuweka majeshi yake katika ardhi ya Kiislamu, katika nchi mbalimbali Mashariki ya Kati.
Alioa mke wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 17 na baadaye akawaoa wake wengine wanne.
Osama Bin Laden anaaminika kuwa na watoto 17.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA