WATU 92 WAFARIKI SAMUNGE

WATU waliofariki Kijiji cha Samunge, wilayani Ngorongoro, kabla ya kupata tiba ya magonjwa sugu inayotolewa na Mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Masapila, wamefikia 92 baada ya wengine sita, wakiwamo raia watatu wa Kenya kufariki wiki hii.
Mganga Mfawidhi Zahanati ya Kata ya Samunge, Dk Elias Lubida, alisema watu sita wamefaniki kuanzia Jumatatu hadi jana.Dk Lubiba aliwataja watu hao kuwa, ni Stain Madokelo, mkazi wa Narock, Jospicke Kipati, mkazi wa Bometi na Lina Chilomo wa Wilaya ya Bomet, Kenya.
Alisema Watanzania waliofariki, ni Ernest Kileo, mkazi wa Hai, Edwin Yusto, mkazi wa Tarime na Sekunda Mmanda, mkazi wa Rombo.
"Wagonjwa hawa walifariki kabla ya kupata kikombe cha tiba, inavyoonekana walifika Samunge wakiwa mahututi," alisema Dk Lubiba.Kuhusu takwimu za waliofariki, Dk Lubiba alisema Aprili walifariki watu wanane na Machi kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Ngorongoro, Dominick Lusasi, watu 78 walifariki.
Lusasi alisema watu hao walifariki kutokana na msongamano uliokuwapo Samunge, hivyo kuzuia wagonjwa waliokuwa mahututi kupata huduma ya kwanza kabla ya kupata kikombe cha tiba.
Vifo hivi vya watu hao, vinaendelea kutokea licha ya serikali na Mchungaji Mwasapila, kutoa taarifa mara kwa mara kushauri wagonjwa mahututi kutopelekwa Samunge.
Mapema wiki hii, Mchungaji Mwasapila aliwataka Wakenya pia kuacha kumpelekea wagonjwa mahututi, ambao wanawaondoa hospitali hasa kutokana na kutokuwa na miundombinu mizuri ya kufika Samunge. Wafuasi 80 wa Chadema Jimbo la Arusha watua Samunge.Wananchi 80 wa Jimbo la Arusha wengi wao wakiwa wanachama wa Chadema, jana walifika Samunge kupata kikombe cha tiba kutokana na ufadhili wa Mbunge wa jimbo hilo, Godbless Lema na Taasisi ya Maendeleo ya Jimbo la Arusha (ArDF).
Wakazi hao wa Arusha, walifika Samunge saa 7:00 mchana, huku wakiimba nyimbo mbalimbali za Chadema.
Katibu Mwenezi wa Chadema Wilaya ya Arusha, Gabriel Lucas, aliyekuwa kiongozi wa msafara huo, alisema wamefarajika kufika Salama Samunge.Lucas alisema katika msafara huo, ambao unatokana na ahadi ya Lema na taasisi yao ArDF, kulikuwa na watu 80 kati yao watoto ni 20.
Naye Mwenyekiti wa ArDF, Elifuraha Mtowe, alisema watu hao 80 kutua Samunge ni awamu ya kwanza na kundi jingine linatarajiwa kufika kesho."Hili ni kundi la kwanza, kundi jingine litafika Samunge Jumapili, tunapenda kutoa shukrani kwa waliofanikisha safari za watu hawa, ambao tunaamini tiba ya babu itawasaidia kuboresha afya zao," alisema Mtowe.
Alisema ArDF na Chadema Arusha, wanampongeza Mchungaji Mwasapila kwa kutoa tiba hiyo kwa gharama ndogo na kuwezesha hata watu wa kipato cha chini kunufaika. Mchungaji Mwasapila ataka wanaokunywa dawa wasiwe malaika.Mchungaji Mwasapila, jana amewataka wagonjwa wanaofika Samunge kupata tiba wasiache kunywa dawa zao wanapougua magonjwa mengine, kwani wao sio malaika. Akizungumza na mamia ya watu kabla ya kuanza kutoa tiba jana, Mchungaji Mwasapila alisema, kama mgonjwa amepata kikombe na baadaye akaugua tena ugonjwa mwingine asisite kwenda hospitali."Ndugu kupata kikombe cha tiba hamjawa malaila, kuwa hamtaugua ugonjwa mwingine tena, kwani kikombe siyo kinga ni tiba hivyo mkiungua nendeni hospitali," alisema Mwasapila.
Alisisitiza kikombe cha tiba ambacho anatoa hakirejewi mara mbili, hivyo wale waliokunywa na sasa wanahisi ugonjwa kurejea wanaweza kurudi Samunge kwa maombi na ushauri mwingine siyo kikombe. Msanii Dude atua Samunge.Msanii maarufu wa kundi la bongo Dar es Salaam, ambalo linarusha michezo yake Kituo cha televisheni cha TBC1, Kulwa Kikumba, maarufu kama Dude jana alitua Samunge na kuwa kivutio.
Dude baada ya kufika Samunge, alishuka kwenye gari na kusalimiana na Mchungaji Mwasapila kicha akapata kikombe na kuondoka.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*