WAZIRI SUDANI AJIUZURU JUU YA MGOGORO WA ABYEI

Nyumba zikichomwa moto Abyei
Waziri wa upande wa kusini mwa Sudan katika serikali ya taifa amejiuzulu, akisema "uhalifu wa kivita" umefanyika katika eneo lenye mzozo la Abyei.
Luka Biong Deng alisema hawezi tena kufanya kazi na chama cha Rais Omar al-Bashir kwenye serikali ya muungano.
Ni afisa mwandamizi kwenye chama tawala cha kusini, kinachotarajiwa kuiongoza Sudan kusini kwenye uhuru wake mwezi Julai.
Pande hizo mbili zimekuwa katika mapambano kwa miongo kadhaa kabla ya kukubali kugawana madaraka na kupiga kura za maoni za kuamua iwapo kusini ijitenge au la.
Nyumba zimechomwa moto Abyei
Wachambuzi wana wasiwasi mzozo huo unaweza kuchochea ghasia za kusini na kaskazini, ambapo takriban watu milioni 1.5 waliuawa.
Majeshi ya kaskazini yaliteka eneo hilo mwishoni mwa juma baada ya majeshi ya kusini kuvamia msafara wa majeshi eneo hilo, na kuua watu 22.
Takriban watu 20,000 kwa sasa wamekimbia mji huo, na kuachwa bila watu, walisema wafanyakazi wa kutoa misaada.
Mkuu wa kutetea haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay alisema alipokea taarifa kuwa majeshi ya kaskazini yamekuwa yakirusha makombora kwa raia.
Bw Biong Deng kwa asili ni mtu wa Abyei, ambapo pande zote mbili zinagombania.


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.