Waziri wa Habari, Vijana, na Michezo, Emmanuel Nchimbi ( kulia)) akimkabidhi Ofisa Michezo wa wizara hiyo, Meja Edwin Mugumba, kombe la timu yenye nidhamu ya JKT Ruvu katika msimu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2010/11 katika hafla ya Vodacom kukabidhi zawadi washindi wa ligi hiyo kwenye ukumbi wa Serengeti katika Hoteli ya Paradise,

Kocha wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 23 'Manyara Stars' Jamhuri kihwelo (kushoto) akimshukuru Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania, George Rwehumbiza baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni 17 za Klabu ya Simba ambayo ilishika nafasi ya pili katika ligi hiyo. Katikati ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah (wa pili kushoto) na Waziri wa Habari, Vijana na Michezo, Emmanuel Nchimbi.






Waziri wa Habari, Vijana, na Michezo, Emmanuel Nchimbi ( wa pili kulia) akimkabidhi Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Yanga, Salumu Rupia, mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni 42 kutoka Kampuni ya Vodacom Tanzania, ikiwa ni zawadi baada ya Yanga kutwaa ubingwa Ligi Kuu ya Vodacom 2010/11. Wanaoshuhudia hafla hiyo iliyofanyika Dar es Salaam ni Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah (wa pili kushoto), Mkuu wa Udhamini wa Vodacom, George Rwehumbiza (wa tatu kushoto) na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Mohamed Bhinda. Picha zaidi uk 23. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)




Baadhi ya viongozi wa Klabu ya Yanga (katikati msitari wa mbele) wakiwa na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Vodacom Tanzania baada ya kukabidhiwa zawadi ya sh. milioni 42 za ubingwa wa Ligi hiyo.






Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen (kushoto) akijadiliana jambo na Kocha wa Timu ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 23, Jamhuri Kihwelo (kulia) pamoja na Kocha wa timu za Taifa za Vijana, Kim Poulsen wakati wa hafla hiyo.









Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*