Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe (aliyevaa suti nyeusi katikati), akiwa na Mbunge Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu (kulia kwake) wakipiga makofi pamoja na wanachama wa kikundi cha Kuweka na Kukopa cha PFT, baada ya kufungua ofisi za kikundi hicho, Tandika, Dar es Salaam

Wasanii wa kikundi cha TMK Wanaume Family wakifanya mashambulizi pamoja na wasanii wa kikundi cha wachekeshaji cha The Orijino Komedy cha TBC, wakati wa hafla ya Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu kukabidhi hundi ya sh. milioni 12 kwa vikundi 27 vya VICOBA pamoja na harambee ya kuchangia mfuko wa kikundi cha PFT. Hafla hiyo ilifanyika jana kwenye viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Dar es Salaam.



Chakawe na wageni wengine wakifurahia shoo hiyo






Wanachama wa kikundi cha VICOBA cha Afya (kushoto), wakifurahia baada ya kupokea hundi ya sh. 444,000 zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (kulia). Anayekabidhi hundi hiyo ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe (aliyevaa miwani).






Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Quality Group, Yusufu Manji (kulia), akijadiliana jambo na Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu (kushoto) pamoja na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Ramadhan Madabida baada ya kuchangia kikundi cha PFT, sh, milioni 20 katika harambee hiyo. Zaidi ya sh, milioni 50 zilichangwa.









Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI