BARAZ\A LA KRIKET ULIMWENGUNI KUTOPUNGUZA TIMU

Timu ya Kenya

Baraza la mchezo wa kriketi ulimwenguni ICC latangaza kwamba limeamua kutupilia mbali hatua ya kuzipunguza timu katika Kombe la Dunia 2015Mataifa kama Kenya, Ireland na Canada, huenda yakanufaika tena kufuatia hatua ya baraza la kriketi ulimwenguni, ICC, kuamua kutupilia mbali wazo la kupunguza timu zitakazoshiriki katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2015, hadi timu 10 tu.
Mwezi Aprili, baraza la ICC lilikuwa limetangaza nia ya kuzipunguza timu hadi 10, kuyaruhusu mataifa wanachama kamili peke yao kupambana katika mashindano hayo.
Baadhi ya wadadi wanasema timu kama Kenya hazipati msaada wa ICC kushirikishwa katika mashindano makubwaIkiwa hatua hiyo ingelitekelezwa, mataifa kama Kenya na Zimbabwe yasingeliweza kushiriki.
Lakini wakuu wa kamati kuu ya mchezo huo ambao wanaendelea na kikao chao cha kila mwaka, wamekubali mashindano hayo yaendelee kuwa na timu 14.
Hayo yanamaanisha kuna mataifa manne ambayo yatajiunga na India, Pakistan, Sri Lanka, Uingereza, Afrika Kusini, New Zealand, Australia, West Indies, Bangladesh na Zimbabwe katika mashindano ya mwaka 2015.
Mbali na Ireland, ambao waliweza kuishinda England katika mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2011, na Pakistan yale ya mwaka 2007, mataifa mengine yasiyokuwa wanachama kamili na yaliyofuzu kushiriki katika mashindano ya mwaka 2011 ilikuwa ni Kenya, Canada na Uholanzi.
Uskochi, ambao walikuwa katika mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 1999 na 2007, walikubali bila ubishi uamuzi wa ICC wa mwezi Aprili kuzipunguza timu hadi 10, lakini walielezea inafaa kuwe na utaratibu fulani wa kuyafanya mataifa yasiyo wanachama kamili kupambana kabla ya kufuzu kushirikishwa katika Kombe la Dunia.
Wazo la kuwa na timu 12 lilijadiliwa katika kamati kuu ya uongozi ya ICC mjini Mumbai, India, mwezi Aprili, lakini wakati huo iliamua kushikilia kwamba timu 10 ni bora.
Wakati huo, aliyekuwa nahodha wa timu ya England, Michael Vaughan, pia alisema ni wazo zuri kuwa na mashindano ya kufuzu.
"Ningelipenda kuona mashindano ya awali ya kufuzu, na mataifa kama Bangladesh na Zimbabwe yakicheza na mataifa kama Ireland, Canada na Kenya na timu za mataifa mengine na timu mbili bora zaidi zikifuzu kwa Kombe la Dunia," alielezea Vaughan.
Lakini licha ya uamuzi huo kuhusiana na mashindano ya mwaka 2015, ICC imethibitisha kwamba mashindano ya mwaka 2019 yatakuwa na timu 10, na 8 zikiwa ndio zinazoongoza katika orodha ya timu bora zaidi kulingana na ICC, na zilizosalia mbili zikiamuliwa kupitia mashindano fulani wa kufuzu.
Kamati kuu ya ICC pia iliidhinisha kuanzishwa kwa utaratibu wa kuzipandisha daraja timu, au kuzishukisha, kama ilivyokuwa imekubaliana juu ya pendekezo hilo hapo awali.
Kamati pia imethibitisha kwamba mashindano ya dunia ya Twenty20 ya mwaka 2012 na 2014 yatakuwa na jumla ya timu 12 (10 za wanachama kamili na mbili za timu zisizokuwa za wanachama kikamilifu).
Huu ndio umekuwa utaratibu wa mashindano hayo tangu yalipoanzishwa mwaka 2007.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI