CHUO KIKUU CHA UDOM CHAFUNGWA KISA MGOMO

Habari tulizozipata kutoka Mkoani Dodoma zinadai kuwa Chuo Kikuu Cha Dodoma-UDOM kitivo cha Sanaa na Sayanzi Jamii na shule ya Sayansi Asilia na Hisabati kimefungwa kwa muda usiojulikana.

Kulingana na Uongozi wa Chuo hicho Kikuu Cha Dodoma wanafunzi hao wamepewa muda wa Masaa Manane wale wameondoka Chuoni hapo.

Kufungwa kwa Chuo hicho Kikuu kunafuatia wanafunzi wa Chuo hicho kuendelea na mgomo wao ndani ya situ Tatu mfululizo wakishnikiza serikali kuwalipa fedha kwa ajili ya kufanya mazoezi kwa vitendo katika vituo mbalimbali nchini .
Wakati huo habari kutoka mkoani Mbeya zinadai kuwa wanafunzi wa chuo cha kilimo Uyole wameanza kulipwa baada ya mgomo wao uliodumu kwa siku saba chuoni hapo.
Habari zilizoufikia mtandao huu kutoka kwa wanafunzi hao zimeeleza kuwa tayari wameanza kulipwa na mhasibu kutoka Wizarani chuoni hapo.
WANAFUNZI hao wamesema wanafunzi 255 wa mwaka wa pili ndiyo wameanza kulipwa kati ya wanachuo 445 wanaosoma katika chuo hicho.
Wanachuo hao waligoma kuingia madarasani kuushinikiza uongozi wa chuo hicho kuwarejeshea michango yao ya Ada waliyotozwa na chuo hicho kimakosa.
Mgomo huo wa amani, ulianza Juni 3 mwaka huu baada ya jitihada za kusuluhisha sakata hilo kushindwa kufikia muafaka kati ya uongozi wa chuo hicho na wanafunzi tangu Mei 19 mwaka huu.
Wakizungumza na mtandao huu katika chuo hicho leo wanafunzi hao walisema kuwa wanakidai chuo hicho zaidi ya Shilingi Milioni Sitini kutokana na kuwatoza ongezeko lisilorasmi la (Michango)Ada zao lililotokana na kikao cha KATC.
Wamesema walitozwa wanatakiwa kurejeshewa kila mmoja Sh. 135,000 kwa wanafunzi wa mwaka wa pili na wanafunzi wa mwaka wa kwanza wanapaswa kurejeshewa Sh.120 kwa kila mmoja hali ambayo imeendelea kuleta mvutano na baadhi ya viongozi wa chuo wanatishiwa kufukuzwa chuo kutokana na ufuatiliaji wa suala hilo.
‘’Sisi tunadai madai yetu halali ambayo hata chuo kinajua kuwa ni halali yetu na ambapo hata chuo cha Ilonga Morogoro walirejeshewa fedha zao hivyo sisi msimamo wetu hatutaingia darasani mapa tupewe fedha zetu ama tuonane na Katibu wa Wizara ya Kilimo na si vinginevyo’’walisemawanafunzi hao.
Mkuu wa chuo hicho Dr, Deonis Limo alikataa kuonana na kuhojiwa na hata kuthubutu kuficha kitabu cha wageni hali iliyojipambanua kuwa kuna jambo linafichika hapo.
Kwa upande wa uongozi wa Serikali ya wanafunzi kupitia Rais wao Ngamenye Kibona, Makamu Noel Msumule, Katibu Deogratius Shilima, Waziri Mkuu Vijinia Mbilinyi na mwakilishi wa Baraza la Mawaziri wa chuo hicho Justine Sevalino wamesema kuwa wameagizwa na uongozi wa chuo hicho kuwa madai ya wanafunzi ya kumtaka Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo hayatatekelezwa na suala la kulipwa fedha hizo watalipwa mwaka wa pili ifikapo Juni 25 mwaka huu siku ya kufunga chuo hicho.
Aidha wamesema wamepewa mtihani mzito wa kuwashawishi wanafunzi wenzao kutii agizo hilo ambalo wanachuo hawalitaki na kwamba cha kushangaza ni kwamba wameelezwa wazi kuwa endapo watashindwa kuwashawishi kukubaliana na maagizo yao basi uongozi huo utakuwa wa kwanza kutimuliwa chuoni hapo ama kuandikiwa sifa mbaya za tabia zao (Character) hali ambayo imewaweka njia panda.
‘’Tumeambiwa Serikali haioni shida kututimua sisi wanafunzi 445 kwa madai kuwa sisi ni wachache hivyo ili kukwepa hilo tunapaswa kusalimu amri na kukubaliana na wanayotaka wao’’ walisema viongozi hao kwa unyonge.
Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa malalamiko ya wanafunzi hao kurejeshewa fedha zao ni halali kutokana na waraka wa Wizara ya Kilimo unaoagiza wanafunzi hao kurejeshewa fedha hizo na warsaka mwingine ambao hauna sahihi unaodhaniwa kugushiwa na baadhi ya viongozi wa chuo hicho.
Waraka huo kutoka Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika ulioandikwa Juni 3 mwaka huu na kupewa kumbukumbu Na; HA355/364/04 una kichwa cha habari Madai ya fedha ya michango ya wanachuo MATI-UYOLE kupito 2009/2010 na 2010/2012 maagizo kutoka Wizarani.
Barua hiyo iliyomlenga mkuu wa chuo hicho imeeleza pia kuwa wanafunzi hao wanatakiwa kurejea madarasani ifikapo Juni 6 mwaka huu(jana) na ambaye hataingia atakuwa amejifukuza chuo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*