Gavana wa benki kuu Afghanistan ajiuzulu

Gavana wa benki kuu nchini Afghanistan Abdul Qadeer Fitrat amejiuzulu kutoka wadhifa huo akihofia maisha yake.
Rais Karzai analaumu washauri wa kigeni kwa hasara iliotokea kwenye benki ya KabulBw Fitrat amsema vigogo serikalini wanamzuia kufanya uchunguzi kuhusu ubadhirifu wa dola nusu bilioni kutoka benki ya Kabul.
Lakini msemaji wa Rais Hamid Karzai, ametaja hatua ya gavana huyo kuwa uhaini mkubwa.
Waheed Omar amesema kuwa uchunguzi ulikuwa umeanzishwa kuhusu utenda kazi wa gavana huyo wa benki kuu.
Uchunguzi umeonyesha kuwa benki hiyo ilitoa mikopo ya mamilioni ya dola bila kufuata maadili, hali iliotishia kuifilisi benki hiyo.
Serikali ya Afghanistan mwaka jana ililazimika kutumia pesa zake kuinusuru benki hiyo.
Rais Karzai aliahidi kuwa uchunguzi utafanyika kuhusu sakata hiyo ya ufujaji wa pesa katika benki hiyo na hatua zitachukuliwa dhidi ya wahusika wote.
Bw Fitrat ambaye sasa yuko uhamishoni, anasema alikuwa na matumaini kuwa uchunguzi huo ungefichua wahusika kwenye sakata hiyo lakini badala yake umechochea matatiza maishani mwake.
"Maisha yangu sasa yamo hatarini. Hii ni baada nilipozungumza bungeni na kufichua watu ambao walihusika na sakata hiyo katika benki ya Kabul" ameelezea Bw Fitrat.
Baadhi ya watu waliotajwa na gavana huyo kuhusika na kashfa hiyo ni ndugu yake Rais Karzai, Mahmoud Karzai.
Idara ya kuchunguza ufisadi nchini Afghanistan ilifichua kuwa zaidi ya dola milioni 467 zilitolewa na benki hiyo kama mikopo kwa vigogo nchini humo bila kufuata utaratibu.
Lakini Rais Karzai alisema nchi yake haina uzoefu wa kutosha kusimamia benki hiyo na amelaumu washauri wa kigeni kwa hasara hiyo iliotokea.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.