KITNE;UTAJIRI WA WACHAHE TZ NI HATARI



Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa katika Serikali ya awamu ya kwanza Dk Hassy Kitine, akizungumza Dar es Salaam jana na washindi wa shindano la shinda 'Nina Ndoto' linaloendeshwa na Kampuni ya Faidika. Picha na Emmanuel Herman ]
Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa katika Serikali ya awamu ya kwanza Dk Hassy Kitine, akizungumza Dar es Salaam jana na washindi wa shindano la shinda 'Nina Ndoto' linaloendeshwa na Kampuni ya Faidika. Picha na Emmanuel HermanMwandishi WetuALIYEWAHI kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa katika Serikali ya awamu ya kwanza Dk Hassy Kitine amesema hali iliyopo sasa nchini ya umaskini mkubwa kwa wananchi inatishia amani.
Kitine ambaye aliwahi pia kuwa mbunge amesema taifa haliwezi kuwa na asilimia moja pekee ya watu wanaoshikilia uchumi wa nchi kama ilivyo sasa Tanzania huku asilimia 99 wakiwa mafukara.
"Watanzania wengi ambao ndiyo wenye nchi hii wanamiliki uchumi kwa asilimia moja tu, huku Watanzania walio chini ya asilimia moja kwa wingi wao wakimiliki uchumi kwa asilimia 99,"alisema Kitine na kuongeza:
“Hali hii inatisha na ni hatari kwa kundi dogo la watu wachache kumiliki uchumi wa Watanzia kwa asilimia 99.“
Mbele ya wanahabari Kitine alisema, "Mnajua napenda kusema, lakini nikisema wengine wanakasirika. Lakini, lazima tusema, Watanzania wengi lazima wamiliki uchumi kikamilifu na si watu wachache."
Akijibu swali kuhusu maandamano yanayoendeshwa na Chadema kupinga hali ngumu ya maisha nchini alisema anakiunga mkono chama hicho akisema kiko sahihi katika kufanya maandamano hayo.
"Hali hiyo ni kitu ambacho kizuri na kinaleta changamoto kwa ‘political parties’ (Vyama vya siasa) na viongozi, kwani hawawezi kufanana, maandamano ni mazuri, ni demokrasia, japo mimi ni mwanachama wa CCM," alisema Kitine.Akizungumzia Serikali ya Awamu ya Tatu iliyoongozwa na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na kipindi cha kwanza cha Serikali ya Awamu ya Nne ya Jakaya Kikwete, Kitine alisema kwamba haoni tofauti katika vipindi hivyo viwili.Hata hivyo, alisema mambo yamekuwa mabaya kutokana na kuondolewa kwa Azimio la Arusha na kwamba uongozi sasa umekuwa wa kununua."Zamani nilipokuwa kiongozi katika Serikali ya Awamu ya Kwanza baada ya kuteuliwa na Rais Nyerere kushika nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Uwaziri na hatimaye Ubunge, uongozi ulikuwa ni ‘dedication’,"alisema.
Alifafanua, "zamani ukitaka kugombea nafasi ya uongozi kama ubunge unaulizwa mali umepata wapi, wenzako wataakuuliza, lakini nikaacha kugombea tena uongozi kutokana hali iliyojitokeza ambayo sasa uongozi unanunuliwa."
Kuhusu kampuni yake ya Faidika amesema hivi sasa inajishugulisha na kuwasaidia wafanyakazi wa sekta ya umma na hapo baadaye itaanza kusaidia pia watu wa sekta binafsi .
Kitime alikuwa akizungumza jijini Dar es Salaam jana wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la pili la ‘shinda ndoto yako’ linaloendeshwa na Kampuni ya Faidika inayojishugulisha na mikopo kwa wafanyakazi wa umma.
Kuhusu kampuni ya Faidika alisema hivi sasa inajishugulisha na kuwasaidia wafanyakazi wa sekta ya umma na hapo baadaye itaanza kusaidia pia watu wa sekta binafsi .
Katika hafla ya jana Mwalimu ya Shule ya Msingi Pongwe iliyopo mkoani Tanga Amiri Ligalwike alikabidhiwa Sh 5 milioni baada ya kuandika mchanganua wake vizuri kuhusu fedha alizokopa sh1.5 milioni jinsi alivyozitumia na kuweza kuboresha maisha yake ya kila siku na jirani zake.Mshindi mwingine ni Makono Andrew aliyeshinda Sh 3 milioni.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI