KUISAKA MAITI YA OSAMA BAHARINI

Kwa kuwa serikali ya Marekani imeshindwa kuwathibitishia watu kuuliwa kwa Osama bin Laden na maiti yake kuzikwa baharini kama wanavyodai, mtaalamu mmoja wa kupiga mbizi baharini wa nchini Marekani amepanga kutumia dola laki nne kuisaka maiti ya Osama bin Laden kwenye bahari ambayo maiti yake ilidaiwa kutupwa.
Bill Warren ambaye ni mtaalamu wa kupiga mbizi baharini mwenye makazi yake mjini San Diego, California nchini Marekani, ameamua kuisaka maiti ya Osama bin Laden baharini ili kujua kama kweli Osama bin Laden aliuliwa na maiti yake ilitupwa baharini.
Akitumia teknolojia za kisasa zilizotumika kuisaka meli ya Titanic, boti za wapiga mbizi na submarine, Warren ametenga dola laki nne kuusaka mwili wa Osama bin Laden baharini.
Kazi ya kuusaka mwili wa Osama itaanza mapema mwezi ujao kwa kuanzia upande wa bahari ya Hindi magharibi mwa India.
Warren mwenye umri wa miaka 59 alipoulizwa sababu ya kutumia pesa zake kuusaka mwili wa Osama alijibu kwa kusema "Nafanya hivi ili kujua kama kweli Osama aliuliwa, tunaamini rais Obama ameshindwa kuwathibitishia watu kuwa Osama bin Laden ameuliwa".
"Nina mpenzi wangu Mrusi ambaye amekuwa akiniambia kuwa Majasusi wa Urusi hawaamini kama Osama bin Laden ameuliwa kweli, mimi simuamini rais Obama wala serikali yake", aliongeza Warren.
"Serikali ya Obama ilitakiwa itoe picha kama ilivyofanya wakati alipouliwa Saddam Hussein", alisema Warren.
Serikali ya Marekani imedai inazo picha za kuuliwa kwa Osama bin Laden ingawa ni wanasiasa wachache sana walichaguliwa kuonyeshwa picha hizo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.