MADEREVA WAZEMBE SASA KUTOZWA SH. 300,000

Joseph ZablonSERIKALI imefanya maboresho katika mfumo kodi 11 tofauti, ikiwamo ile ya usalama barabarani baada ya kupandisha faini kwa mtu anayepatikana na kosa kutoka Sh20,00 hadi Sh50,000.Hatua hiyo ya serikali inadaiwa itapunguza makosa ya barabarani na ajali zinazotokana na uzembe.
Akiwasilisha bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2011/2012 bungeni Dodoma jana, Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo, alisema mabadiliko hayo ya faini yametokana na kufanyiwa marekebisho sheria namba ya usalama barabarani.
“Napendekeza kufanya marekebisho ya Sheria ya Usalama Barabarani, Sura 168 ili kuongeza ukomo wa kiwango cha faini inayotozwa kwa kufanya makosa wakati wa uendeshaji gari barabarani kutoka Sh20, 000 hadi Sh50,000” alisema.
Sheria zingine ambazo zimefanyiwa marekebisho, ni ile ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), Sheria ya Kodi ya Mapato, Ushuru wa bidhaa, Sheria ya Elimu ya Mafunzo na Ufundi Stadi.
Mkulo alitaja sheria zingine kuwa, ni ushuru wa stempu, ushuru wa mafuta na ile ya petroli, leseni za biashara na marekebisho ya ada na tozo mbalimbali za wizara, mikoa na idara zinazojitegemea.
Waziri Mkullo alisema serikali itaendelea kuchukua hatua mbalimbali za sera na utawala, ili kuongeza mapato ya kodi na yasiyo ya kodi, kupanua wigo wa mapato maeneo mengine.
Pia, serikali imesamehe kodi ya mapato kwenye posho wanazolipwa wafanyakazi wa serikali na wanaofanya kazi kwenye taasisi zinazopata ruzuku kutoka serikalini.
Alisema serikali itaendelea kupitia sheria mbalimbali zinazotoa misamaha ya kodi kwa lengo la kuidhibiti, kusimamia mpango wa tatu wa Miaka mitano ya maboresho ya utendaji kazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuendelea kuingiza sekta isiyo rasmi kwenye mfumo wa kodi.
Pia, serikali inapitia upya mfumo wa ukusanyaji kodi ya majengo kwenye majiji, miji, manispaa, wilaya na miji midogo; kufanya mapitio ya vyanzo vya mapato na mfumo wa ukusanyaji katika serikali za mitaa, ili kuongeza mapato.
Kuhusu marekebisho kodi zingine ikiwamo VAT, Mkullo alisema yamefanyika ili kuhamasisha uwekezaji na kuboresha uzalishaji sekta za kilimo, mifugo, viwanda, biashara na utalii.
Alisema kulingana na maboresho hayo, serikali imesamehe kodi ya ongezeko la thamani kwenye vipuri vya zana za kilimo; fyekeo, mashine za kukausha na kukoboa mpunga, mashine za kupandia mbegu na matrekta ya kukokota kwa mkono (power tillers).
“Lengo ni kuhamasisha matumizi ya zana bora za kilimo na kuvutia uwekezaji kwenye sekta ya kilimo, hatua ya kusamehe VAT kwenye chakula cha kuku inalengo la kuhamasisha uwekezaji nchini,” alisema.Kodi zingine zimeondolewa katika nyuzi zinazotumika kutengenezea nyavu za kuvulia samaki, vipuri vya mashine za kunyunyizia na kutifua udongo na mashine za kupanda nafaka.
Pia, imeanzisha utaratibu wa marejesho ya kodi kwenye mauzo rejareja kwa bidhaa za ndani zinazouzwa kwa abiria, ambao siyo raia wa Tanzania wanaosafiri nje ya nchi.


Comments

NI ULAJI MZURI KWA POLISI.POLISI OYEEEE MMEPEWA ULAJI NA MADREZA WATACHAGUA MOJA KULIPA LAKI TATU AU KUMPA POLISI 50000.
jiulize hivi polisi wa usalama barabarani wanaingizia serikali sh ngapi kwa mwezi mapato ya faini.
INGEKUWA KWELI BASI MADREZA WANGEWEZA KUPUNGUZA AJALI

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA