MBUNGE SAKAYA ARUDISHWA RUMANDE

MBUNGE wa Viti Maalumu kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Magdalena Sakaya pamoja na wenzake 10, jana walirudishwa tena rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana waliyopewa na mahakama.
Masharti waliyopewa washtakiwa hao yaligawanyika katika sehemu mbili yakiwatofautisha wale wanaotoka ndani ya Wilaya ya Urambo pamoja na wale wanaotoka nje ya wilaya hiyo.
Kwa wale wanaotoka nje ya Wilaya ya Urambo akiwamo, Mbunge Magdalena Sakaya walipewa masharti ya kupata hati ya mali isiyohamishika pamoja na kusaini dhamana ya Sh 3milioni huku wale wanaotoka ndani ya wilaya wakitakiwa kupeleka barua ya ofisa mtendaji wa kata.
Washtakiwa wote walishindwa kutimiza masharti na walirudishwa rumande ambapo Hakimu Mkazi, Oscar Bulugu aliahirisha kesi hadi Juni 20 mwezi huu shauri lao litakapotajwa tena.
Kabla ya washtakiwa hao kupandishwa kizimbani kulikuwa na makundi ya watu ambao wengi wanadaiwa ni wafuasi wa CUF waliokuwa wakifuatilia shauri hilo wakiwa na imani kuwa washtakiwa watapata dhamana.
Kufuatia makundi ya watu hata idadi ya polisi nayo ilikuwa kubwa kuimarisha ulinzi wa kutosha kukabiliana na aina yoyote ya vurugu endapo ingetokea mahakamani hapo.
Pamoja na baadhi ya watu kuhangaika kuhakikisha washtakiwa hao wanapata dhamana, jitihada zao zilikwama huku wengine wakisikika wakidai kuwa endapo viongozi wa kitaifa wa chama hicho wangekuwepo huenda washtakiwa wangepata dhamana.
Washtakiwa wote 11 akiwamo Mbunge Sakaya, walifikishwa wiki iliyopita baada ya kukamatwa karibu wiki mbili zilizopita ambapo walirudishwa rumande hadi jana.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.