MISRI HAITAKI FAINALI KOMBE LA MATAIFA



Waandalizi wa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2006, Misri, ambao si tu walikuwa wenyeji, bali walichukua kombe pia, wamesema hawana nia ya kuwa wenyeji wa mashindano ya mwaka 2013, kutokana na matatizo yanayoendelea Libya.Kulingana na makamu wa rais wa chama cha soka cha EFA nchini Misri, Hany Abou-Reida, nchi yake haina mipango ya kuwa mwenyeji.Kutokana na wenyeji Libya kujipata katika vurugu la kisiasa na raia kutaka kumuondoa Muammar Gaddafi uongozini, kumekuwa na shinikizo kwamba mashindano hayo yafanyike katika nchi nyingine.Afrika Kusini tayari imeelezea nia yake ya kuwa mwenyeji wa fainali hizo za 2013. Misri ilitwaa ubingwa mwaka 2006 ilipokuwa mwenyeji wa Kombe la Mataifa ya AfrikaAlgeria pia imeelezea kwamba ingelitaka kuwa mwenyeji wa mashindano hayo, ambayo yatazishirikisha timu 16 za Afrika.Katibu mkuu wa shirikisho la soka barani Afrika, CAF, Hichal El Amrani, ameielezea BBC kwamba kamati kuu ya shirikisho hilo la mataifa ya Afrika itakuwa na kikao mjini Cairo, mwezi Septemba, na kujadiliana zaidi kuhusu hali ilivyo nchini Libya.Kumekuwa na gumzo kwamba Misri, walioandaa mashindano ya mwaka 2006, watashindania nafasi hiyo ya kuhakikisha mashindano hayo yatafanyika katika taifa la Afrika ya kaskazini.Lakini Abou-Reida, akihojiwa na gazeti la Al Ahram, alisema Misri haina nia ya kuwa mwenyeji. Abou-Reida alisema: "Kama raia yeyote wa Misri nilitazamia nchi yangu ingelipata heshima ya kuandaa mashindano hayo, lakini kimsingi hatupo kwa kuwa sisi tulikuwa wenyeji wa mashindano ya mwaka 2006."

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.