MKURUGENZI WA TAZARA ATIWA KIZIMBANI DAR

Hussein IssaMKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania na Zambia (Tazara ), Akashambatwa Lewanika amekamatwa na Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam kwa kosa la kutohudhuria mahakamani aliposhitakiwa na wastaafu wa shirika hilo.Kukamatwa kwa mkurugenzi huyo kumefanya shughuli za kiutendaji kusimama kwa muda katika shirika hilo, baada ya maafisa wote kuhamia Kituo cha Polisi Chang’ombe.
Kwa mujibu wa habari ambazo Mwananchi ilizipata, mkurugenzi huyo alikamatwa jana asubuhi ofisini kwake huku wafanyakazi wastaafu wakishangilia kukamatwa kwake.
Chanzo cha habari kilisema kwamba mkurugenzi huyo hajawahi kutokea mahakamani wala kutuma mwakilishi tangu kuanza kwa kesi hiyo kati ya shirika hilo na wastaafu wanaodai fidia zao.Chanzo hicho cha habari kilisema kwamba kutokana na dharau hiyo ndiyo maana Jeshi la Polisi lilipomtia nguvuni kiongozi huyo.
Kamanda wa Jeshi Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime alisema kwamba yeye hana taarifa ya kukamatwa kwa mkurugenzi huyo kwa sababu alikuwa katika mkutano tangu asubuhi.“Kwa kweli sijui lolote, mimi tangu asubuhi nilikuwa katika mkutano na makamanda wenzangu,”alisema Misime.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI