MKUU WA MAJESHI ASHANGAA KULIPWA PENSHENI SH 50,000

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange (kushoto) akiwa na Rais Jakaya Kikwete wakati wa sherehe za Muungano.

Filbert Rweyemamu, Arusha


MKUU wa Majeshi ya Ulinzi mstaafu, Jenerali Mirisho Sarakikya ameitaka serikali kuangalia upya maslahi ya wanajeshi wastaafu akisema bado wanayo nafasi ya kulitumikia taifa kwani bado ni askari wa akiba kwa mujibu wa viapo vyao.
Akihutubia katika uzinduzi wa Muungano wa Wanajeshi Wastaafu Tanzania (Muwawata), Mkoa wa Arusha, alisema yeye pamoja na kulitumikia jeshi kwa muda mrefu, ameweza kujenga kibanda cha kuishi yeye na familia yake huku akilipwa pensheni ya Sh50,000 kwa mwezi lakini akiwaona baadhi ya watumishi wa umma wakiwa na majengo ya kifahari katika miji mbalimbali nchini.
“Kuna watumishi wana majengo ya makubwa ambayo hayaendani na mapato yao, nasema haya kwa sababu tunajua mishahara yao haiendani na maisha na mali walizonazo. Hivyo wastaafu wenzangu, msitegemee miujiza, umoja huu ndiyo utakuwa mkombozi kupigania maslahi yenu,” alisema Sarakikya.
Alisema mbali na kuwa mtumishi wa umma hadi mwaka 1974 na kisha kuingia kwenye siasa akiwa Mbunge wa Jimbo la Arumeru na mwaka 1977 kuteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria na baadaye Ethiopia na Kenya, baada ya kustaafu analipwa Sh50,000 kwa mwezi.
“Nyie wastaafu wa hivi karibuni najua pensheni zenu nzuri kuliko ya kwangu, kwa hiyo jambo la msingi huu muungano ni muhimu sana ili kuhakikisha mnajinasua na ugumu wa maisha,” alisema.
Aliongeza kuwa serikali na jeshi wafanye utafiti, kujua ni kazi gani zinazoweza kufanywa na wanajeshi wastaafu na wapewe kipaumbele kutokana na kuwa wanajeshi wasitaafu kulingana na vyeo vyao na wala si umri kama watumishi wengine wa umma.“Naomba serikali na jeshi jambo la kwanza liwe ni kwenda katika nchi nyingine wafanye utafiti ili kujua zinafanya nini juu ya wastaafu wao, kisha wampe ushauri CDF (Mkuu wa Majeshi) jambo la kufanya,” alisema Sarakikya.
Mwenyekiti wa Taifa wa Muwawata, Sajenti Taji Assedd Mayugi alisema lengo lao ni kujikomboa kiuchumi na kutekeleza maagizo ya serikali ya kuwa jeshi la akiba.Alisema wakiwa ni wataalamu wa masuala mbalimbali ukiwamo ulinzi, wanaitaka serikali ione umuhimu wa kuwapa maeneo ya ulinzi ya serikali ili siri zake zisivuje ovyo.
Akizindua muungano huo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isdore Shirima alisema serikali itayafanyia kazi mapendelezo ya wastaafu hayo.ameshangazwa na utajiri wa kutisha wa baadhi ya watendaji wa Serikali usiolingana na kipato chao, huku akiitaka serikali kuangalia upya hali ya kiuchumi ya wanajeshi wastaafu.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA