MRWANDA, KASSIM WAITWA STARS

WACHEZAJI MRWANDA, KASSIMDan Mrwanda na Abdi Kassim ni miongoni wa wachezaji saba wanaocheza mpira wa kulipwa nje ya nchi walioitwa na kocha wa Taifa Stars, Jan Poulsen kwa ajili ya mechi dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati itakayofanyika Juni 5 mwaka huu jijini Bangui. Klabu yao ya Dong Tam Long ya Vietnam imekataa kuwaruhusu wachezaji hao kujiunga na Stars kwa madai kuwa iko kwenye hali ngumu katika ligi yao. Timu hiyo inashika nafasi ya mwisho kwenye ligi ya nchi hiyo inayoshirikisha timu 14, hivyo kudai kuwa wachezaji hao ni muhimu kwao kuwaokoa kutoka mkiani. TFF tumepinga hatua hiyo kwa vile ni kinyume na Kanuni ya Hadhi na Uhamisho wa Wachezaji (Regulations of Status and Players Transfer), hivyo tutawasilisha malalamiko yetu kwa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI