MWALIMU AOZESHWA MKE MAITI KABLA YA KUZIKWA USIKU

Mazishi yakiendelea majira ya 3.45 usiku kwa kutumia mwanga wa taa na tochi za simu baada ya kupatikana kwa makubaliano kwa mme kukubali kuozeshwa maiti ya mkewe





Mkuu wa shule ya Star mjini Iringa Jesca Msambatavangu ambaye ni kada wa CCM (kulia) akiwa ameshika spedi kusaidia kufukia mwili wa marehemu Magreth Ray Mng'ong'o





Diwani wa kata ya Mvinjeni Frank Nyalusi (chadema) wa pili kulia akiwa ameongozana na ndugu wa marehemu na wananchi wakitoka kuzika majira ya saa 4 kasoro usiku. (PICHA ZA BLOGU YA FRANCIS GODWIN)








Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Filauni ni methali ambayo ni ngumu kuielewa iwapo halijakukuta la kukukuta ila kwa waliopatwa kukutwa kwao si methali japo si wengi wamekutana na methali hii ila kwa mwalimu Raymond Twanzihilwa wa shule ya msingi Ipogolo mjini Iringa kwake methali hii imetimia .
Kifo cha Mkewe Magreth Raymond Mng'ong'o (40) kimeweza kumthibitishia kuwa dunia ni watu na kuwa watu na viatu wasio penda ya watu baada ya leo kujikuta katika wakati mgumu zaidi baada ya baba mkwe wake kutaka kaburi lifukuliwe na maiti kurudishwa nyumbani eneo la kitwiru ili mwalimu huyo aweze kukamilisha kulipa mahali kabla ya mwili huo kuzikwa .
Utata huu ulianza majira ya saa 2 asubuhi wakati taratibu za mazishi zikifanyika na wananchi wakiwa katika harakati za kwenda kuchimba kaburi ili kumzika maheremu huyo aliyefariki ghafla kwa ugonjwa na BP akiwa nyumbani kwake Kitwiru mjini Iringa.
Baba Mkwe wa mwalimu Ray aliuambia mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com ambao ulipata kushuhudia tukio hilo LIVE kuwa mwalimu huyo hakukamilisha mahali wakati akimuoa binti yake hivyo yeye kama baba mzazi hakuwa tayari mwili huo kuzikwa Iringa kabla ya kutolewa mahali na hivyo kutaka maiti hiyo kufukuliwa ili ikazikwe Kilimanjaro kwa ngudu zake ama Njombe ambako ni nyumbani alikozaliwa marehemu huyo na kuwa iwapo watalazimisha mwili huo kuzikwa hapo wasishangae kuukuta mwili huo katika nyumba za wale walioshiriki kuzika.
Mwalimu Ray mwenyewe akizungumza na mtandao huu alisem akuwa mzee huyo alimfanyia unyanyasaji wa hali ya juu kwani mahali yote alikuwa ameitoa toka mwaka 1990 alipomuoa mwanamke huyo na sehemu ya mahali iliyobaki ambayo ni shilingi 90,000 baba mkwe alifika Iringa na kuomba kupewa baiskeli .
Hata hivyo alisema kutokana na hatua ya mzee huyo kung'ang'ania mahali mbele za watu na kuzuia maiti hiyo kuzikwa ndipo kwa upande wake alipoamua kujifungia ndani ya nyumba yake na kutaka kujiua kabla ya wananchi kufika na kumlipia mahali ya shilingi 500,000 na ushehe .
Viongozi wa serikali ya mtaa huo wa Kitwiru na diwani wa kata ya Kitwiru Ally Mbata walisema kuwa kutokana na mgogolo huo walilazimika kutoa taarifa polisi ili kuomba ulinzi zaidi eneo hilo baada ya baadhi ya vijana kuanza kuishambulia kwa mawe nyumba yenye maiti kama njia ya kupinga hatua ya baba mkwe kutoza mahali maiti .
Huku diwani wa kata ya Mvinjeni Frank Nyalusi akisema kuwa alifanya jitihada za kupiga simu polisi ili kuomba ulinzi japo hajapendezwa na hatua ya polisi kuchelewa kufika eneo hilo.
Mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com ulishuhudia mazishi ya marehemu huyo yakifanyika bila ibada kama ilivyokuwa awali huku vijana wakifukia kaburi kwa kutumia mikono bila jembe wala spedi kwa takribani dakika 20 hivi kabla ya vifaa hivyo kupatikana .
Mwanga wa taa za chemli na toshi ndizo zilizotumika kuongeza mwanga makaburini hapo huku mbalamwezi iliyokuwepo awali ikionekana kufifia baada ya kujitokeza hali ya kisayansi katika mwezi huo na ghafla kutokea kiza katika eneo hilo.
Baada ya kurejea kutoka kuzika majira ya saa 4 usiku na mfiwa mwalimu Ray kuwashukuru wananchi zaidi ya 200 waliojitokeza kuzika maiti hiyo ,wananchi hao hasa vijana walifunga kwa muda barabara kuu ya Iringa-Mbeya huku wakizuia magari kupita likiwemo gari ya askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa Dr Owdernburg Mdegella ambaye alikuwa akitokea upande wa Mafinga kuja Iringa mjini.









Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU