NYAMLANI ATEULIWA MJUMBE CAF

Nyamlani akiwa na Rais Jakaya Kikwete katika hafla moja Ikulu, Dar es Salaam
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Athumani Nyamlani ameteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Rufani ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF). Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu wa CAF, Hicham El Amrani iliyotumwa kwa Nyamlani jana, kikao kinachofuata cha Kamati hiyo kitafanyika Septemba 25 mwaka huu makao makuu ya shirikisho hilo jijini Cairo, Misri. Nyamlani ambaye kitaaluma ni mwanasheria anakuwa Mtanzania wa kwanza kuingia katika kamati hiyo. Pia ni kiongozi wa mpira wa miguu kwa muda mrefu akianzia Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Temeke (TEFA), Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na kilichokuwa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT) sasa TFF. Boniface WamburaOfisa Habari

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU